Mafundi wa Mizani kutoka Wakala wa Mizani mkoa wa Simiyu wakikagua mizani ya kununulia pamba
****
Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.
WAKALA wa Mizani (WMA) Mkoa wa Simiyu imekagua jumla ya Mizani 638 kwa ajili ya ununuzi wa Pamba katika msimu wa 2022/23 kutoka kwa makampuni mbalimbali ya ununuzi wa pamba pamoja na vyama vya ushirika (Amcos).
Hayo yamebainishwa leo na Kaimu Meneja wa Wakala wa Mizani Mkoa huo, Tuntufye Mkumbo wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake waliotaka kufahamu namna Wakala huyo anavyohusika kukagua mizani ya wanunuzi wa Pamba.
Amesema hadi sasa wanaendelea na zoezi la uhakiki wa Mizani katika wilaya zote za mkoa wa Simiyu na mara baada ya kuhakiki mizani, watapita vijijini kukagua usahihi wa mizani hiyo kama ambavyo waliikagua.
‘’Tumehakiki mizani 638 mpaka sasa kwa mkoa wa Simiyu, Vyama vya Ushirika (Amcos) mizani 359 na makapuni binafsi tumekagua mizani 249, tumekagua kampuni za Alliance ginnery, Vitrex, NGS, Remei, Sm Holdings….zoezi la uhakiki wa mizani lilikuwa linasuasua kwa sababu Amcos walikuwa hawajui kama wananunua pamba au la!’’amesema Mkumbo.
Mkumbo amesema majukumu ya wakala wa vipimo ni kuhakiki vipimo vyote ambavyo vinatumika katika maeneo mbalimbali, pia wanatakiwa kusimamia usahihi wa mizani na vipimo hivyo hususani kwenye maeneo ya biashara.
‘’Kuna mizani mingine inahakikiwa sehemu za baridi, haiwezi kuwa sawa na iliyohakikiwa kwenye maeneo ya joto…kingine binadamu anaweza kuichezea mizani kwa lengo la kuwaibiwa wakulima au walaji, mizani inaweza kuchezewa au kuharibiwa na mtu yoyote’’ amesema.
Mkumbo amewaonya wanunuzi wote watakaonunua pamba bila mizani kukaguliwa kwa watakuwa wanakwepa haki kwa wakulima pia wanaweza kuwa wanajipunja wenyewe bila kujua, pia amewaonya maafisa vipimo wanaojihusisha kuharibu mizani kuwa watachukulia hatua za kisheria.
Meneja Mkumbo amesema amepewa mamlaka ya kisheria ya kumfifirisha endapo mtuhumiwa akikiri kosa la kuharibu mzani ambapo atapigwa faini ya shilingi laki moja mpaka miliobi 20 na endapo hatakiri atapelekwa mahakamani kwa ajili ya hatua za kisheria.
Amewataka wanunuzi wote wahakikishe mizani yao imekaguliwa na endapo utakutwa mzani haujakaguliwa watachukuliwa hatua ikiwemo kukamatwa na kufikishwa mahakamani, ambapo amewataka kuwasilisha mizani kwa ajili ya ukaguzi.
‘’Huwa tunaweka seal na stika kwenye mzani, tunapokuwa tunapita katika ukaguzi tunaangalia nani hajahakiki au amekata steal, Je, stika ipo…..ili mtu achezee mzani lazima akate steal, tukikuta haipo tunamchukulia hatua…’’ amesema Mkumbo.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Mizani Mkoa wa Simiyu Tuntufye Mkumbo akiwaonyesha stika na steal waandishi wa habari (hawapo pichani) namna wanavyofungua ili isiharibiwa.
Fundi wa Mizani kutoka Wakala wa Mizani Mkoa wa Simiyu Abdallah Kasili akirekebisha mzani wa kununulia Pamba.
Social Plugin