************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KLABU ya Yanga imeondoka na ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya timu ya Mbeya Kwanza, gimu ambayo inashika mkia kwenye ligi ya NBC.
Ni Fiston Kalala Mayele, baada ya mechi nne mfululizo kukosa kufunga bao leo ameonesha kuwa anaweza mara baada ya kupachika bao la kwanza kwenye mchenzo huo na kufikia mabao 14 akiwa sambamba na mchezaji wa Geita Gold George Mpole.
Yanga Sc imebakiza mechi mbili kuweza kutangazwa bingwa wa ligi ya NBC ambapo mpaka sasa anaongoza ligi akiwa imejikusanyia pointi 63 nyuma ya Simba Sc mwenye alama 50.
Mabao mengine ya Yanga Sc yamewekwa kimyani na Said Ntibazokiza, Dikson Ambundo na bao la mwisho likifungwa na Makambo.
Social Plugin