***********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KLABU ya Yanga imeendelea kutoa sare ambapo leo imelazimishwa sare na timu ya Tanzania Prison mchezo uliochezwa katika dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Yanga Sc imechezea nafasi nyingi za wazi kipindi cha kwanza licha ya kupata penati ambayo ilienda kupigwa na mshambuliaji wao Fiston Mayele lakini hakuweza kufunga na mpira ukaenda juu.
Yanga huu mchezo wake wa tatu mfululizo wanashindwa kupata ushindi baada ya mechi waliocheza na Simba Sc na kutoka sarre ya bila kufungana na mechi ya pili ambayo ilichezwa mkoani Kigoma dhidi ya Ruvu Shooting nako alitoa sare ya bila kufungana.
Yanga Sc sasa itakuwa imeiiacha Simba kwa alama 11 huku Simba akiwa na mchezo mmoja mkononi
Social Plugin