Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imetiliana saini hati ya makubaliano kutengeneza mfumo wa kuwatambua watanzania wanaoishi nje ya nchi, utakaofahamika kama 'Diaspora Digital Hub', ambao utagharimu jumla ya shilingi milioni 100 zitakazotolewa na Benki ya CRDB, utajumuisha watoa huduma wa Serikali kama; NIDA, UHAMIAJI & TIC pamoja na watoa huduma wengine ambao huduma zao zinawalenga Diaspora.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela kwa pamoja na Katibu Mkuu Wizara la Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine, wakitiliana saini hati ya makubaliano baina ya Benki ya CRDB na Wizara kwa ajili ya utengenezaji wa mfumo wa kidigitali kwa Wantazania waishio nje ya nchi (Diaspora), utakaowawezesha kupata huduma mbalimbali wanazohitaji kutoka nyumbani Tanzania wakiwa hukohuko ughaibuni. Mfumo huo utajumuisha watoa huduma wa Serikali kama; NIDA, UHAMIAJI & TIC pamoja na watoa huduma wengine ambao huduma zao zinawalenga Diaspora. Hafla hiyo imefanyila leo kwenye ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni wanasheria wa pande zote mbili wakishuhudia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela kwa pamoja na Katibu Mkuu Wizara la Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine, wakibadilishana hati za makubaliano baina ya Benki ya CRDB na Wizara baada ya kuzisiani kwa ajili ya utengenezaji wa mfumo wa kidigitali jijini DSM ambapo jumla ya shilingi milioni 100 zimetolewa na benki hiyo kuwezesha mfumo huo kwa Wantazania waishio nje ya nchi (Diaspora), ambao utawawezesha kupata huduma mbalimbali wanazohitaji kutoka nyumbani Tanzania wakiwa hukohuko ughaibuni. Mfumo huo utajumuisha watoa huduma wa Serikali kama; NIDA, UHAMIAJI & TIC pamoja na watoa huduma wengine ambao huduma zao zinawalenga Diaspora. Hafla hiyo imefanyila leo kwenye ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa na kulia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora cha Wizara Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi James Bwana,
Katibu Mkuu Wizara la Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akizungumza katika hafla fupi ya kusaini makubaliano baina ya Benki ya CRDB na Wizara kwa ajili ya utengenezaji wa mfumo wa kidigitali, ambao utawawezesha watanzania waishio nje ya nchi kupata huduma mbalimbali wanazohitaji kutoka nyumbani Tanzania wakiwa hukohuko ughaibuni. Mfumo huo ambao utagharimu jumla ya shilingi milioni 100 zitakazotolewa na Benki ya CRDB, utajumuisha watoa huduma wa Serikali kama; NIDA, UHAMIAJI & TIC pamoja na watoa huduma wengine ambao huduma zao zinawalenga Diaspora. Hafla hiyo imefanyila mwishoni mwa wiki kwenye ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza katika hafla fupi ya kusaini makubaliano baina ya Benki ya CRDB na Wizara kwa ajili ya utengenezaji wa mfumo wa kidigitali, ambao utawawezesha watanzania waishio nje ya nchi (Diaspora), kupata huduma mbalimbali wanazohitaji kutoka nyumbani Tanzania wakiwa hukohuko ughaibuni. Mfumo huo ambao utagharimu jumla ya shilingi milioni 100 zitakazotolewa na Benki ya CRDB, utajumuisha watoa huduma wa Serikali kama; NIDA, UHAMIAJI & TIC pamoja na watoa huduma wengine ambao huduma zao zinawalenga Diaspora. Hafla hiyo imefanyila leo kwenye ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, jijini Dar es salaam.