Chongolo Alisema hayo katika uwanja wa ndege wa Kigoma majira ya saa 11 jioni
alipowasili Mkoani Kigoma akiwa njiani kuelekea Nchini Burundi akiongozana na Viongozi wengine wa chama hicho Taifa, Wilaya na Mkoa Kigoma, ambapo alitarajia kupokelewa na Wenyeji wake Mpakani mwa Tanzania na Burundi Manyovu Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma jioni leo.
Katika Ziara yake Nchini Burundi Katibu mkuu Chongolo atakagua Uwanja wa Mpira uliojengwa Mkoa wa Makamba Nchini Burundi, ambao unaomiklikiwa na Katibu Mkuu wa CNDD-FDD, Reverien Ndikuriyo uwanja huo pia una kituo cha kukuza vipaji.
Alisema kuwa uwanja huo utakuwa chachu katika kuibua vipaji kwa wanamichezo nchini Burundi lakini pia itajuwa fursa kubwa kwa Watanzania kutumia nafasi hiyo kwa wanamichezo wake kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji vya wanamichezo wake chipukizi hasa wa mkoa Kigoma.
“MKOA wa Kigoma Unahitaji kupata timu ya ligi kuu kwa hio huu ushirikiano kati ya Tanzania na Burundi Kupitia Michezo, utakuwa mwanzo mzuri wa kufanikisha mkoa Kigoma kuwa na timu ya ligi kuu kwenye soka sambamba na michezo mingine,"alisema Chongolo
aliongeza Kuwa Mkoa wa Kigoma Una vipaji Vingi na kwamba kutakuwa na mwendelezo wa ligi itakayohusisha mikoa ya Burundi na Mkoa wa Kigoma kwa lengo la kuibua vipaji, na kuwezesha ajira na kujenga afya kupitia michezo na vijana wengi wakae mkao wa kula burudani kupitia michezo.
Aidha aliongeza kuwa Kukamilika kwa Uwanja wa Mpira Wa Makamba nchini Burundi ni chachu kwa Chama hicho kuboresha uwanja wake wa Lake Tanganyika uliopo mkoani Kigoma wa kuendeela kuboresha ili kuweka uwiano wa viwanja vitakavyo endelea kukidhi mahitaji muhimu ya kimichezo kwa nchi hizo na ligi za ndani.
Uwanja huo pia ndiyo uwanjani wa nyumbani na makao makuu ya timu ya Eagle Noir (Black Eagle) inayocheza ligi kuu ya nchini Burundi
Katibu Mkuu wa CCM anatarajia kufika Bujumbura nchini Burundi ambapo atakuwa na mazungumzo na viongozi wa CNDD- FDD.
Alisema kuwa ziara hiyo inafanyika kwa Mwaliko wa Katibu Mkuu wa CNDD- FDD ambaye ameshafanya ziara mara tatu nchini Tanzania.
Social Plugin