Mkazi wa Maswa, mkoani Simiyu, Salum Nkonja maarufu kama Emmanuel Nkonja, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka 11 yakiwemo kukutwa na chuchu za binadamu, sehemu za siri tano za wanawake na mafuvu mawili ya kichwa cha binadamu.
Nkonja amefikishwa mahakamani hapo leo, Juni 21, 2022 na kusomewa kesi ya uhujumu uchumi namba 32/2022 na wakili wa Serikali, Caroline Materu, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Ramadhani Rugemalira.
Chanzo - Mwananchi
Social Plugin