Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

'HUSBAND MATERIAL' ANASWA AKIFUA NGUO ZA NDANI ZA MPENZI WAKE KWA UMAKINI MKUBWA...GUMZO MTANDAONI

 Mrembo mmoja amemuanika mpenzi wake ambaye alikuwa anaosha chupi zake kwenye video inayozagaa mtandaoni. 


Katika video hiyo, mwanaume huyo anaonyeshwa akifua chupi za mrembo wake ambaye alikuwa amevaa tabasamu tele usoni kando yake.

 

Alikuwa akiziosha kwa makini na kusugua uchafu, kung'arisha akiwa amechangamka na kufurahia kazi yake. 


Katika njia ya kujivunia mpenzi wake, mrembo huyo alimrekodi kwenye video akiwa amejaa tabasamu akisema: "Ona mpenzi wangu", akizungusha kamera kila upande. 


Alitaka kutangazia ulimwengu mzima maana ya "husband material" bila ya jamaa huyo kutambua kile kilikuwa kinaendelea na kusikika akimuuliza mrembo huyo endapo chupi aliyoshika mkononi ni aina ya "G-string".


 Punde jamaa huyo alipotambua kuwa mrembo wake alikuwa anamrekodi, alichana mbuga na kuficha uso wake. 


Katika taarifa nyingine ,Mwanaume mmoja kutoka nchini Ghana mwenye umri ya kati alinaswa kwenye video ambayo inasambazwa sana mitandaoni akiosha nguo za ndani za mke wake na kufunza umma namna ya kutekeleza shughuli hiyo. 


Alikuwa ameketi kwenye kiti nje ya nyumba yake, akiwa ameinama huku akiosha kwa makini chupi za mke wake na kuwasimulia wanaume namna ya kuzingatia mambo kadhaa.


 Jamaa huyo Alielezewa kama aibu kwa waume wenzake huku wanawake wakimtaja kama mwanamume ambaye anajali. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com