Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : WAZAZI SHULE ZA HOPE WAFANYA SHEREHE 'HOPE DAY' KUPONGEZANA, KUJADILI KUPAISHA ZAIDI TAALUMA

Mgeni Rasmi Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Justin Kaziulaya akitoa vyeti kwa wazazi ambao wamekuwa vinara wa kutoa ushirikiano wa kutosha shuleni hapo.
Mkurugenzi wa Shule za Hope Bahati Dede akizunguma kwenye sherehe hiyo ya wazazi shuleni hapo.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

SHULE binafsi ya Hope iliyopo Lubaga Manispaa ya Shinyanga ambayo inatoa elimu kuanzia awali, msingi hadi Sekondari imefanya sherehe ya kukutana na wazazi ambao wanasomesha watoto wao shuleni hapo, kubadilishana mawazo namna kuboresha taaluma shuleni hapo na kufurahi pamoja.

Shule hiyo ya Hope imekuwa ikifanya vizuri kitaaluma ambapo kiwilaya ya Shinyanga imekuwa ikishika nafasi ya kwanza pamoja na kuendelea kufanya vizuri pia kimkoa na kitaifa, na kuwataka wazazi wawapeleke watoto wao kupata elimu bora katika shule hiyo.

Mkuu wa Shule ya Hope Extended Excellence Secondary Alphonce John, amesema shule ya Hope ilianzishwa mwaka 2002 na sasa ina miaka 20 na imekuwa ikifanya vizuri kitaaluma, kutokana na ushirikiano mzuri na wazazi kwa kupeana mawazo namna ya uboreshaji wa elimu.

“Shule hii ya Hope ina miaka 20 sasa ambapo tulianza na utoaji wa elimu ya awali na msingi, lakini sasa hivi tumepanua utoaji wa elimu na kuanzisha shule ya Sekondari na sasa tupo ngazi ya kidato cha tatu na mwakani wanafunzi wanaingia kidato cha nne,”amesema John.

“Tunawashukuru wazazi kwa kuendelea kutuunga mkono na kutoa mawazo yenu namna ya kuboresha utoaji wa taaluma, na tumekuwa tukifanya vizuri kwa sababu yenu na watoto wamekuwa wakitimiza ndoto zao na tunawaomba muendelee kuwa mabalozi wazuri wa kuitangaza shule yetu,”ameongeza.

Naye Mkurugenzi wa shule za Hope Bahati Dede amewapongeza wazazi kwa kuitika kwa wingi kuhudhuria sherehe hiyo ambayo imewakutanisha na kujadili mambo mbalimbali ya kitaaluma na kuwasihi waendelee na ushirikiano huo ili kuwapatia elimu bora watoto wao na kuja kuwa viongozi wakubwa katika Taifa.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Justin Kaziulaya, ameipongeza shule kwa kukutana na wazazi ikiwa maendeleo mazuri ya wanafunzi shuleni yanahitaji ushirikiano wa pande zote wazazi pamoja na walimu.

Katika hatua nyingine ametoa wito kwa wazazi mkoani Shinyanga siku ya zoezi la kuhesabiwa Sensa ya watu na makazi ambalo litafanyika Agost 23 mwaka huu washiriki kikamilifu ili zoezi hilo lifanikiwe pamoja na kujitokeza kwenye Mbio za Mwenge wa Uhuru. 

Nao baadhi ya wazazi ambao wanasomesha watoto wao shuleni hapo wamepongeza utaratibu huo wa kukutana na walimu na kujadiliana masuala mbalimbali ya uboreshaji wa taaluma na hatimaye watoto wao kufanya vizuri kielimu.

Mkurugenzi wa Shule za Hope Bahati Dede akizunguma kwenye sherehe hiyo ya wazazi shuleni hapo.

Mgeni Rasmi Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Justin Kaziulaya,akizungumza kwenye sherehe hiyo ya wazazi.
Mkuu wa Shule ya Hope Extended Excellence Secondary Alphonce John, akisoma taarifa ya shule.

Mwanafunzi Rosemary Amoni akisoma Risala ya Shule.

Mgeni Rasmi Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Justin Kaziulaya, akikata keki kwenye sherehe hiyo ya wazazi katika shule ya Hope.

Muonekano wa keki.

Wanafunzi wa Hope Extended Excellence Secondary School wakiwa kwenye sherehe ya wazazi shuleni hapo.

Wanafunzi wa Hope Extended Excellence Secondary School wakiwa kwenye sherehe ya wazazi shuleni hapo.

Wanafunzi wa awali na msingi wa shule ya Hope wakiwa kwenye sherehe hizo.

Wazazi wakiwa kwenye sherehe yao.

Sherehe ikiendelea.

Sherehe ikiendelea.

Sherehe ikiendelea.

Sherehe ikiendelea.

Sherehe ikiendelea.

Sherehe ikiendelea.

Burudani za ubunifu wa mitindo wa mavazi zkiendelea kwenye sherehe hizo.

Burudani za ubunifu wa mitindo wa mavazi ukiendelea kwenye sherehe hizo.

Burudani za ubunifu wa mitindo wa mavazi zikiendelea kwenye sherehe hizo.

Burudani zikiendelea kwenye sherehe hizo.

Burudani zikiendelea kwenye sherehe hizo.

Burudani zikiendelea kwenye sherehe hizo.

Burudani zikiendelea kwenye sherehe hizo.

Mashindano ya uvaaji Tsheti yaliendelea kwenye sherehe hizo.

Mashindano ya ujazaji maji kwenye chupa yakiendelea.

Mashindano ya uvaaji viatu yakiendelea kwenye sherehe hizo.

Mashindano ya uvutaji Kamba yakiendelea kwenye sherehe hizo kati ya wazazi (kushoto) na walimu (kulia) ambapo walimu waliibuka na ushindi.

Mgeni Rasmi Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Justin Kaziulaya akitoa vyeti kwa wazazi ambao wamekuwa vinara wa kutoa ushirikiano wa kutosha shuleni hapo.

Mgeni Rasmi Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Justin Kaziulaya akitoa vyeti kwa wazazi ambao wamekuwa vinara wa kutoa ushirikiano wa kutosha shuleni hapo.

Mgeni Rasmi Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Justin Kaziulaya akitoa vyeti kwa wazazi ambao wamekuwa vinara wa kutoa ushirikiano wa kutosha shuleni hapo.

Mgeni Rasmi Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Justin Kaziulaya akitoa vyeti kwa wazazi ambao wamekuwa vinara wa kutoa ushirikiano wa kutosha shuleni hapo.

Mgeni Rasmi Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Justin Kaziulaya akitoa vyeti kwa wazazi ambao wamekuwa vinara wa kutoa ushirikiano wa kutosha shuleni hapo.

Mgeni Rasmi Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Justin Kaziulaya akitoa vyeti kwa wazazi ambao wamekuwa vinara wa kutoa ushirikiano wa kutosha shuleni hapo.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com