MAFUNZO YA UJUZI TEPE KWA MAKUNDI MAALUMU YA VIJANA YAZINDULIWA RASMI SHINYANGA…WAPEWA MBINU ZA KUJIKWAMUA KIUCHUMI

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Beda Chamatata akizungumza wakati akizindua Mafunzo Tepe (Soft Skills) kwa Makundi Maalumu ya Vijana Wenye Ulemavu, wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (WAVIU) na Wamama Wadogo (Young Mothers) yanayohusu masuala ya Ujasiriamali, Usimamizi wa Biashara, Kujitambua, Afya ya Uzazi na Ujinsia uliofanyika katika Ukumbi wa Liga Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga tarehe 29 Juni, 2022.

Na Chiku Makwai Shinyanga.

OFISI ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), imetoa mafunzo ya ujuzi tepe (Soft Skills) kwa makundi maalumu ya vijana, wakiwamo wenye ulemavu, wamama wadogo (Young Mothers) na wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (WAVIU) katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa lengo la kuwawezesha kujitambua na kujitathmini.

Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Liga Hotel Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ambapo vijana takribani 75 wamefundishwa mada mbalimbali ikiwemo ujasiriamali usimamizi wa biashara, kujitambua, Afya ya uzazi na ujinsia.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ya siku tatu (Juni 28,2022 hadi Juni 30,2022, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Beda Chamatata amesema suala la vijana kutokuwa na elimu ya ujuzi tepe, limekuwa likisababisha vijana kukabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwamo za kiuchumi, kiafya pamoja na kupata mimba katika umri mdogo na kupoteza dira ya maisha yao.

Amesema kuwa mafunzo hayo ya ujuzi tepe yatakuwa msaada mkubwa kwa vijana hao katika kujitambua, na kufanya maamuzi sahihi juu ya masuala mbalimbali katika maisha yao na kuweza kuzifikia ndoto zao.

Aidha ameipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuanzisha Programu ya kutoa Mafunzo ya Ujuzi tepe kwa makundi maalumu ya vijana ambayo ni muhimu kwa mustakabali wa maisha ya vijana.

“Programu hii ya ujuzi tepe ni muhimu sana kwa Taifa letu, itawasaidia vijana waondokane na mazingira ambayo huwapelekea kutokuwa na mwelekeo wa maisha, ambapo watasimama imara na kutimiza ndoto zao” amesema Chamatata.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Rajabu Masanche, amewaasa vijana hao watakapomaliza mafunzo yao na kuunda vikundi vya ujasiriamali, watumie pia fursa za kupata mikopo ya Halmashauri asilimia 10, ambapo asilimia nne hutolewa kwa wanawake na 4% kwa vijana, na asilimia mbili kwa watu wenye ulemavu, ili wapate mitaji na kuanzisha biashara zao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Julius Tweneshe, amesema malengo ya mafunzo hayo ni kuwawezesha vijana kiuchumi pamoja na kuwaonyesha fursa mbalimbali ambazo zinapatikana zikiwemo za mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana uliopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Nao Baadhi ya vijana ambao wamepata mafunzo hayo, akiwamo Happnes Kasembo, amesema mafunzo hayo yamewasaidia kupata elimu ya kujitambua, pamoja na kufanya maamuzi sahihi kwa manufaa wa maisha yao, na kufanya shughuli mbalimbali za kuwaingizia kipato na kuacha kuwa tegemezi ikiwa tayari wameshapatiwa mwanga wa maisha na kuziishi ndoto zao.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Beda Chamatata akizungumza wakati akizindua Mafunzo Tepe (Soft Skills) kwa Makundi Maalumu ya Vijana Wenye Ulemavu, wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (WAVIU) na Wamama Wadogo (Young Mothers) yanayohusu masuala ya Ujasiriamali, Usimamizi wa Biashara, Kujitambua, Afya ya Uzazi na Ujinsia uliofanyika katika Ukumbi wa Liga Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga tarehe 29 Juni, 2022.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Beda Chamatata akizungumza wakati akizindua Mafunzo Tepe (Soft Skills) kwa Makundi Maalumu ya Vijana Wenye Ulemavu, wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (WAVIU) na Wamama Wadogo (Young Mothers) yanayohusu masuala ya Ujasiriamali, Usimamizi wa Biashara, Kujitambua, Afya ya Uzazi na Ujinsia uliofanyika katika Ukumbi wa Liga Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga tarehe 29 Juni, 2022.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Julius Tweneshe akizungumza wakati Uzinduzi wa Mafunzo Tepe (Soft Skills) kwa Makundi Maalumu ya Vijana Wenye Ulemavu, wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (WAVIU) na Wamama Wadogo (Young Mothers) yanayohusu masuala ya Ujasiriamali, Usimamizi wa Biashara, Kujitambua, Afya ya Uzazi na Ujinsia yanayofanyika katika Ukumbi wa Liga Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga tarehe 29 Juni, 2022.

Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Idara ya Maendeleo ya Vijana Godfrey Massawe akizungumza wakati wa Uzinduzi Mafunzo Tepe (Soft Skills) yaliyofanyika katika ukumbi wa Liga Hotel Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Rajabu Masanche akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Mafunzo Tepe (Soft Skills) kwa Makundi Maalumu ya Vijana Wenye Ulemavu, wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (WAVIU) na Wamama Wadogo (Young Mothers) yanayohusu masuala ya Ujasiriamali, Usimamizi wa Biashara, Kujitambua, Afya ya Uzazi na Ujinsia uliofanyika katika Ukumbi wa Liga Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga tarehe 29 Juni, 2022.
Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Ester Makune akizungumza wakati wa Uzinduzi Mafunzo Tepe (Soft Skills) yaliyofanyika katika ukumbi wa Liga Hotel Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Mwakilishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Godfrey Kajia akizungumza wakati wa Uzinduzi Mafunzo Tepe (Soft Skills) yaliyofanyika katika ukumbi wa Liga Hotel Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Mafunzo Tepe, Rose Joel akizungumza wakati wa Uzinduzi Mafunzo Tepe (Soft Skills) yaliyofanyika katika ukumbi wa Liga Hotel Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Beda Chamatata (kushoto) Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Julius Tweneshe (katikati) na Mwenyekiti wa Mafunzo Tepe, Rose Joel  wakiwa kwenye Uzinduzi Mafunzo Tepe (Soft Skills) yaliyofanyika katika ukumbi wa Liga Hotel Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Sehemu ya Vijana Waliohudhuria Uzinduzi wa Mafunzo Tepe (Soft Skills) kwa Makundi Maalumu ya Vijana Wenye Ulemavu, WAVIU na Wamama Wadogo (Young Mothers) yanayohusu masuala ya Ujasiriamali, Usimamizi wa Biashara, Kujitambua, Afya ya Uzazi na Ujinsia kwa lengo la kuwajengea uelewa kwenye masuala hayo yanayofanyika katika Ukumbi wa Liga Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga tarehe 29 Juni, 2022.
Sehemu ya Vijana Waliohudhuria Uzinduzi wa Mafunzo Tepe (Soft Skills) kwa Makundi Maalumu ya Vijana Wenye Ulemavu, WAVIU na Wamama Wadogo (Young Mothers)

PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU,
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post