Picha haihusiani na habari hapa chini
**
Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linawashikilia watu watatu ambao ni ndugu wa mama mmoja kwa tuhuma za kushirikiana na kumuua mama yao mzazi Milembe Lutubija (70) mkazi wa Kijiji cha Nyaruyeye, Kata ya Nyaruyeye ,Tarafa ya Busanda Wilaya ya Geita.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Kamishna Msaidizi Henry Mwaibambe amesema tukio limetokea Juni 1,2022 Majira ya Saa Moja Jioni.
Ameeleza kuwa watoto wa marehemu ambao ni Jumbe Kifoda(36),Dotto Kifoda(34) na Lukina Kifoda(30) walishirikiana na kumuua mama yao kwa kumkata na kitu chenye makali kichwani na mikono ya kulia na kushoto na kusababisha kifo chake.
Mwaibambe amesema kuwa Mama yao aliwataka watoto wake waondoke kwake ili waende kujitegemea lakini watoto hao wakawa wanashinikiza kugawiwa ardhi ya shamba ambalo lilikuwa ni mali ya Mama huyo na marehemu mume wake.
Kamanda Mwaibambe ameongeza kuwa mwenendo wa watuhumiwa hao ukionyesha kuwa walikuwa wanaahidi mara kwa mara kumuua mama yao kwasababu ya kuwafukuza kwenye shamba hilo.
Kwa mujibu wa Kamanda Mwaibambe watuhumiwa wote wamekamatwa na baada ya Upelelezi kukamilika watafukishwa mahakamani.
Social Plugin