Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam linamshikilia mwanaume mmoja aitwaye Heri Julius Kisaka wa miaka 33 ambaye ni fundi simu na mkazi wa Mburahati kwa tuhuma za mauaji ya mwanamke msusi.
Akithibitisha kushikiliwa kwa mtuhumiwa huyo kamanda wa Jeshi la polisi Kanda maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro amesema mtuhumiwa huyo anadaiwa kumuua mwanamke aitwaye Leonia Julius Zerota anayekadiriwa kuwa na miaka 30-33 msusi maeneo ya Sinza, Kinondoni.
Amesema tukio hilo lilitokea Juni 17, 2022 katika moja ya chumba kwenye nyumba ya kulala wageni iitwayo Lavi Park iliyopo Tegeta kwa Ndevu ambapo mwili wa marehemu ulikutwa ndani ya chumba hicho.
Kamanda amesema mtuhumiwa baada ya kutekeleza mauaji hayo alifanikiwa kutoroka na ufuatiliaji ulipoanza alikamatwa akiwa maeneo ya Manzese Jijini Dar es salaam.
Hata hivyo kamanda Jumanne Muliro amesema chanzo cha mauaji hayo bado kinachunguzwa.
Social Plugin