Mfano wa mavazi tata
Mwenyekiti wa Mtaa wa Dome Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Solomoni Najulwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
MWENYEKITI wa Mtaa wa Dome Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Solomoni Najulwa, ameendesha mkutano wa hadhara wa kupiga vita madawa ya kulevya na matukio ya ukatili wa kijinsia, huku wazee wa mtaa huo wakilalamikia mavazi ya wasichana ya nusu utupu kuwa yamekuwa na mitego na kusababisha kufanyiwa ukatili.
Mkutano huo wa hadhara umefanyika Juni 23, 2022 kwenye viwanja vya mirunda katika Mtaa huo wa Dome, huku ukihudhuliwa na Maofisa wa Jeshi la Polisi kwa ajili ya kutoa elimu ya masuala ya ulinzi na usalama, kupiga vita biashara na matumizi ya madawa ya kulevya, pamoja na matukio ya ukatili wa kijinsia.
Baadhi ya wazee ambao walihudhuria mkutano huo akiwamo Robert Mwelo, amesema moja ya tatizo ambalo limekuwa likisababisha matukio ya ukatili wa kijinsia kuendelea ndani ya jamii hasa kwa wasichana inasababishwa na uvaaji wa mavazi yao na nusu utupu.
“Mavazi ya wasichana wetu ya nusu uchi ndiyo chanzo cha matukio haya ya ukatili, unajua wanawake ni kama sumaku wewe unamuona binti kavaa nusu uchi harafu anatembea huku akitingisha mimi nikimuona naanza kufikiria nimvae nini maana ananitega, na kwa mavazi haya ya uchi mtafunga wanaume wengi sana,”amesema Mwelo.
Naye Mwananchi Misipina Misana aliunga mkono kulaani mavazi ya nusu uchi kwa wasichana, huku akibainisha kuwa jamii pia imekuwa ikishindwa kutoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia hasa kwa watoto wa majirani kwa sababu ya kuogopa uhasama.
Akizungumza kwenye Mkutano huo Mwenyekiti wa Mtaa wa Dome Solomoni Najulwa, amesema wameendesha mkutano huo ili kutoa elimu kwa wananchi, kuachana na vitendo vya uhalifu ili jamii iishi salama kwa amani na utulivu na kufanya shughuli zao za kimaendeleo bila ya bughuza yoyote.
“Mtaa huu wa Dome tunataka uendelee na kuwa mfano kwa mitaa yote hapa Shinyanga, hatutaki fujo wala matukio ya uharifu tunataka watu waishi kwa amani na utulivu wala kusikwepo matukio ya ukatili wa kijinsia bali amani itawale,”amesema Najulwa.
“Tumekuwa tukipiga vita uuzaji wa madawa ya kulevya na matumizi hasa kwa vijana, pamoja na kuzuia matukio ya ukatili wa kijinsia, lakini kuna baadhi ya watu wachache bado wanaendeleza vitendo hivi ndiyo maana leo tumeamua kuitisha mkutano huu ili kutoa elimu zaidi,”ameongeza.
Aidha, amesema mbali na kupiga vita matukio hayo ya uhalifu, pia Mtaa huo wa Dome wamefanya vitu vingi vya maendeleo, ikiwamo kusimamia akina mama na vijana na watu wenye ulemavu kupata mikopo ya halmashauri asilimia kumi, msahama wa matibabu bure kwa wazee, kutatua migogoro mbalimbali pamoja na kuimarisha usafi wa mazingira.
Kwa upande wake Mratibu wa dawati la jinsia kutoka Jeshi la Polisi Wilaya ya Shinyanga Brighton Rutajama, akitoa elimu ya ukatili wa kijinsia ,amewataka wananchi kutofumbia macho vitendo hivyo bali wawe wanatoa taarifa na ushahidi mahakamani ili wahusika wachukuliwe hatua kali za kisheria ndipo vitendo hivyo vitakoma.
Naye Mratibu wa Polisi Jamii Wilaya ya Shinyanga Osward Nyorobi, amewasihi wazazi mkoani Shinyanga kujenga pia tabia ya kukagua watoto wao kila mara kabla ya kulala ili kuona kama hawajafanyiwa vitendo vya ukatili, pamoja na kuwa makini na wageni majumbani mwao sababu matukio mengi ya ukatili hufanywa na watu wa karibu.
Katika hatua nyingine amemtaka mtu ambaye anajihusisha na uuzaji wa madawa ya kulevya katika Mtaa huo wa Dome aliyemtaja wa jina la Juma ajisalimishe haraka sana Polisi kabla ya kutumia nguvu kumkamata.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Dome Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Solomoni Najulwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Dome Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Solomoni Najulwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara.
Mratibu wa Dawati la Jinsia kutoka Jeshi la Polisi wilaya Brighton Rutajama, akitoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwenye mkutano huo.
Mratibu wa Polisi Jamii wilaya ya Shinyanga Osward Nyorobi,akitoa elimu ya ulinzi na usalama kwenye mkutano huo.
Wananchi wakizungumza kwenye mkutano huo, kulia ni Mzee Robert Mwelo na kushoto ni Misipina Misana.
Wananchi wa Mtaa wa Dome Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mkutano wa hadhara.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Wananchi wa Mtaa wa Dome Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mkutano wa hadhara.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA.
Social Plugin