JAMAA ATUPWA JELA KISA KAOA MKE WA PILI BILA RUHUSA YA MKE WA KWANZA

 

Mahakama ya Pakistan imemuhukumu mwanaume kifungo cha miezi sita kwa kuoa mke wa pili bila ruhusa ya mke wa kwanza.


Mke wa mwanaume huyo kwa jina Saqib, Bi Ayesha Bibi, alishinda kesi hiyo, alipodai kuwa kitendo cha mume wake kuoa mke wa pili bila yeye kumpatia ruhusa ya maandishi , kilikuw ani ukiukaji wa sheria ya familia nchini Pakistan.

Jaji ali,muamuru mwanaume huyo kulipa faini ya dola 2,000.

Watetezi wa haki za wanawake wanasema uamuzi huo wa mahakama utawazuwia wanawake kuoa wake zaidi ya mmoja. Pia wanasema kuwa utawajengea uwezo na kuwawezesha wanawake kwernda mahakamani kudai haki yao.

"Inatia moyo kwamba mwanamke aliyenyanyaswa amelipeleka hili mahakamani," alisema Romana Bashir, kuu wa mradi wa amani na maendelea nchini humo. "Uamuazi huu unawapa uwezo wanawake," aliongeza.

Nchini Pakistan wanaume wanaweza kuoa wake wengine, lakini ni lazima waombe idhini kwa mke wa kwanza kabla ya kuoa mke mwingine.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post