Ukosefu wa nguvu za kiume ni tatizo la kusikitisha linaloweza kuvunja nyumba nyingi.
Huku idadi kubwa ya tatizo hilo likihusishwa na maradhi au matatizo ya kiafya, utafiti umeonyesha mambo na tabia za kila siku za wanaume zinazoweza kuchangia hali hiyo.
Zifuatazo ni tabia za kila siku ambazo huenda zinamaliza nguvu zako za kiume na kuathiri afya yako ya kushiriki ngono bila wewe kujua.
1. Kuvuta sigara
Matangazo ya sigara huandamana kila mara na ilani kuwa ‘uvutaji wa sigara unadhuru afya yako’, wengi hupuuza na kuendelea na tabia hiyo.
Kando na kusababisha saratani, uvutaji sigara hupunguza mbegu za uume na huweza kuathiri utendakazi wako chumbani.
2. Unywaji Pombe
Unywaji pombe kupita kiasi ni tabia inayoweza kuharibu vibaya afya ya mwanamume kuhusu uzazi. Japo huonekana kama tabia ya kila siku isiyo na madhara, madhara yake kwa uzazi na kushiriki ngono yanasikitisha.
Usihadaiwe na msisimko wake wa muda mfupi.
3. Kuvalia kaptula zinazobana
Hili ni jambo linalopuuzwa na wanaume wengi. Hamna haja ya kuweka bidhaa yako muhimu ikiwa imesakamwa na mavazi ya kubana, valia size yako! Vazi linalofaa ni linaloruhusu kiungo chako kupumua bila kukisakama hali inayoathiri utekelezaji wako na nguvu za uzazi.
4. Msongo wa mawazo
Hali hii inaweza kutatiza afya yako kwa jumla. Tenga muda wa kupunguza mawazo, usiwaze mno. Fanya kazi kwa bidii lakini uwe na muda wa kupumzisha mwili na akili.
5. Vyakula visivyofaa
Lishe bora ni muhimu mno kwa afya ya mwanamume,. Usile tu chakula kingi, kula chakula kinachofaa, jaribu kusawazisha kila viinimwili.
6. Matumizi ya mihadarati
Mihadarati kama vile bangi na nyinginezo huweza kuathiri kihasi nguvu za kiume. Wengi hujihusisha nayo pasipo kujua madhara yake. Wanaume, ikiwa unahusika na mojawapo wa tabia hizi, usife moyo. Kuna mbinu nyingi za kurekebisha hali hii ama kwa kuacha au kupunguza kinachosababisha.