Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SIMIYU WAANZA KUNUFAIKA NA MFUMO WA NI -KONEKT KUPATA HUDUMA ZA UMEME


Mhandisi Innocent Kates kutoka TANESCO akiwa anaunganisha umeme kwenye nyumba ya mteja aliyewashiwa umeme wilayani Bariadi mkoa wa Simiyu.
Fundi umeme Elia Samwel akiwa juu ya nguzo wakati wa zoezi la kuunganisha na kuwawashia umeme majumbani.
Afisa Uhusiano kwa umma TANESCO Simiyu Pilli Mbasha akiwaelimisha wananchi kuhusu mfumo wa Ni - konekt.

Na Samirah Yusuph - Simiyu

Wakazi wa mkoa wa Simiyu wamenza kunufaika na huduma ya Ni- konekt kupitia simu za mkononi na komputa inayotolewa na shirika la umeme TANESCO mkoani Simiyu ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za umeme kwa wateja.

Akitoa elimu kwa wananchi leo Juni 8,2022 Afisa Uhusiano kwa umma Tanesco Mkoa wa Simiyu Pilli Mbasha amesema huduma hiyo imeanza kutumika tangu june 6 na tayari baadhi ya wateja waliotuma maombi kuipitia mfumo huo wamepatiwa huduma na hata kuwashiwa umeme.

Pilli amesema mfumo huo umerahisisha huduma ya usajili kwa wateja wapya na hakuna mzunguko wa kufata huduma za usajili katika ofisi za Tanesco.

“Mwanzo ilikuwa ni ngumu kumuelewesha mteja aliyeomba umeme miezi mitatu iliyopita kuwa bado tunafanyia kazi ombi lake hali kuwa haoni umeme ukiwaka nyumbani kwake lakini kwa sasa mteja naomba mwenyewe na taarifa ya kinachoendelea katika ombi lake anaweza kuiona kila anapohitaji”, amesema pilli.

Amesema katika hatua za awali tangu kuanza kwa huduma ya Ni- konekt tayari wateja wawii waliotuma maombi June 6 leo wamewashiwa umeme na wanaendelea kupata huduma hivyo bado dawati la huduma kwa wateja wanaendelea kutoa elimu kwa umma ili kila mwenye uhitaji aombe kupitia mfumo huo.

Mbuta Masasi ni mmoja kati ya wateja wawili waliowashiwa umeme kupitia maombi yaliyotumia mfumo wa Ni- konekt amesema haikuchukua masaa 24 ili kuwashiwa umeme na hiyo inategemea mtandao wa siku aliyoomba haukusumbua.

“Nimefanya maombi leo baada ya kukamilisha nimefanya malipo na wamekuja kuniwashia umeme hivyo mfumo huu nimeuelewa kuwa ni kweli umelenga kuturahisishia huduma wateja,” amesema Mbuta.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com