Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Lilian Liundi Lilian akiwasilisha sera ya jinsia kwa vyama vya siasa .
Meza kuu katika mkutano wa katika ya uongozi ya vyama vya siasa na TGNP
wajumbe wa kikao cha mashauriano na baraza la vyama vya siasa
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini,Bwa.Sistyl Nyahoza akichangia mada kweye mkutano wa uongozi wa vyama vya siasa.
Ikiwa ni mwendelezo wa majadiliano na mashauriano na Baraza la Vyama vya Siasa juu ya kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi wa kisiasa na ngazi za maamuzi, TGNP na WiLDAF
wakutana na kamati ya uongozi wa Vyama vya Siasa kukubaliana mapendekezo ya kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi wa siasa.
Kikao hiki kitakachofuatiwa na kikao cha Baraza zima la Vyama vya Siasa hapo kesho tarehe 13 Juni kinafanyika mjini Unguja Zanzibar.
**
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na Shirika la WiLDAF kwa ufadhili wa UK Aid, wamekutana na kamati ya Uongozi wa vyama vya siasa nchini kujadiliana namna bora ya kuongeza ushiriki wa wanawake katika ngazi za maamuzi na Uongozi katika vyama vya siasa kama sehemu ya uhamasishaji wa utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa kipengele cha 6A na 6B.
Kikao hicho kilichofanyika leo Juni 12, 2022 katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar, ni mwendelezo wa vikao vya Mashauriano na Baraza vilivyofanyika mwezi Februari mwaka huu ambavyo vilitoka na mapendekezo ya namna ya kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi na ngazi za maamuzi.
Katika kikao cha leo kamati ya Uongozi wa Baraza umeyajadili kwa kina mapendekezo hayo na kukubaliana kuyawasilisha katika baraza kubwa la Vyama vya Siasa ili kupitisha kwa hatua zaidi za utekelezaji.
Miongoni mwa mapendekezo yaliyojadiliwa ni pamoja na Vyama vya Siasa kuwa na Sera ya Jinsia na Mfumo mahususi wa kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi wa siasa.
Kikao hicho cha mashauriano kitaendelea kesho, tarehe 13 Juni 2022 ambapo mapendekezo hayo yatawasilishwa kwa wajumbe wote wa Vyama vya Siasa kupitishwa kwa hatua zaidi.
Social Plugin