Mwanaume mmoja kutoka kaunti ya Kilifi nchini Kenya anayehusishwa na mauaji ya mkewe ametiwa mbaroni na sasa anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Mtwapa.
Mwanaume huyo ambaye ni dereva wa lori anadaiwa kurejea kutoka safarini na kufanya kitendo hicho cha kinyama baada ya mkewe kupokea simu majira ya saa sita usiku.
Ripoti ya NTV ilionyesha kuwa Lulu Ibrahim mwenye umri wa miaka 29 ambaye alikuwa mama wa watoto sita alikata roho kutokana na majeraha mabaya aliyopata.
Ndugu zake walishindwa kustahimili uchungu wao walipoupokea mwili wa jamaa yao na kulaani tukio hilo wakijutia kutokuwa na imani kubwa kati ya mume na mkewe.
Social Plugin