Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KAMPUNI YA TBL YAAHIDI MAKUBWA USIKU WA WADAU WA HABARI KANDA YA HABARI




Na Mwandishi wetu - Mwanza

Kampuni ya bia ya TBL imewataka wadau  mbalimbali wa habari  Mkoani Mwanza  kushiriki mara kwa mara kwenye usiku wa waandishi wa habari na wadau wa habari Kanda ya Ziwa kwani kuna fursa kubwa ya kutangaza huduma na bidhaa zao.

Hayo yamezungumzwa na Meneja Mauzo wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Yuda Ryaga alipotembelewa na waandishi wa habari leo kiwandani hapo ikiwa ni maandalizi ya kuelekea siku ya usiku wa Waandishi na Wadau wa habari Ijumaa June 3 mwaka huu.

"Ningependa sana kuona siku hiyo ya waandishi wa habari kama bidhaa zote zitakuwa mezani ili wanahabari wapate nafasi ya kuonja bidhaa zetu na tunawahakikishia tu kwamba tushirikiane pamoja" amesema Ryaga.

Ameongeza kuwa jamii inayoizunguka kiwanda hicho imeendelea kunufaika kwa kupata ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kwa maana kwamba ndani ya kiwanda kuna makampuni mengine madogo madogo ambayo yamechukua kazi ndogo ndogo ikiwemo usafi, huduma ya chakula ambao wengi waajiriwa ni wakazi wa Mwanza lakini pia wanatoa huduma ya maji ya kunywa.

"Kiwanda pia kinatoa pia huduma ya maji safi na salama ya kunywa kwa ajili ya wakazi wanaozunguka kiwanda na tunafungua  saa 12 aubuhi na kufunga saa 12 jioni ili watu waweze kupata maji safi na salama kwa matumizu ya nyumbani," amesema Ryaga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com