Haya siyo mafuriko! Bali ni Bomba kubwa la Maji la mm 300 la Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) linalopita katika eneo la Stendi ya Soko Kuu Mjini Shinyanga likiwa limepasuka baada ya kuharibiwa kwa bahati mbaya na mtambo wa kuchonga barabara (Greda) uliokuwa unang’oa kisiki jirani na nguzo ya umeme katika eneo ambalo ujenzi wa stendi ya Soko Kuu unaendelea.
Tukio hilo limetokea leo Jumamosi Juni 18,2022 majira ya saa 12 jioni ambapo maji hayo yametiririka kuelekea maeneo mbalimbali mjini Shinyanga kwa takribani saa moja na kusababisha uharibifu/uhalifu wa mazingira na upotevu mkubwa wa maji.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka SHUWASA baadhi ya maeneo mjini Shinyanga yatakosa huduma ya maji wakati wa kushughulikia tatizo hilo lililotokea.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Tazama Video hapa chini
Moja kati ya visiki kilichokuwa kinaondolewa jirani na nguzo ya umeme
Moja kati ya visiki kilichokuwa kinaondolewa jirani na nguzo ya umeme
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog