MAGHETO CHANZO CHA UKATILI WA KIJINSIA …WANAFUNZI LUNGUYA SEKONDARI WAVUNGA KURIPOTI HOFU YA VITISHO, KUROGWA

Afisa Kiongozi wa Programu TGNP, Bi. Joyce Mkina akiongoza Mdahalo kwa vijana wa kiume katika shule ya Sekondari Lunguya iliyopo katika kata ya Lunguya halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga wenye lengo la kujadili namna kuzuia ukatili wa kijinsia shuleni na ndani ya jamii.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Wanafunzi wa kiume wanaosoma katika shule ya Sekondari Lunguya iliyopo katika kata ya Lunguya halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga wamesema nyumba za kupanga ‘magheto’ kwa wanafunzi ni kichocheo cha matukio ya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa kike hali inayochangia mimba na ndoa za utotoni.

Wameyasema hayo leo Ijumaa Juni 10,2022 shuleni hapo wakati wa mdahalo kuhusu namna ya kuzuia ukatili wa kijinsia shuleni na ndani ya jamii ulioandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la UNFPA kwa ufadhili wa KOICA.

Wakizungumza katika mdahalo huo wanafunzi hao wa kiume wamesema wanafunzi wa kike wanaoishi wenye nyumba za kupanga ‘magheto’ wanakuwa na uhuru sana hivyo ni rahisi kuingia kwenye vishawishi matokeo yake wanajiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi na wanaume na kusababisha kupata mimba na kuolewa.

“Miongoni mwa mambo mengine yanayochochea ukatili wa kijinsia ni pamoja na wanafunzi wa kiume kutumika kuwaunganishia wanaume wa mtaani wanafunzi wenzao wa kike hivyo wanafunzi kujikuta tayari wameanza mahusiano ya kimapenzi na kupoteza ndoto zao”,wamesema wanafunzi hao.

“Kuna baadhi ya wanapewa pesa na wanaume wa mtaani wawasaidie kutongoza/kuwapelekea wanafunzi wa kike, wanatumwa na kaka zao, marafiki na watu mbalimbali kuwaitia wanafunzi wa kike hii inachangia matukio ya ukatili wa kijinsia. Tumepata elimu ya madhara ya ukatili wa kijinsia sasa hatutatumika tena kushiriki matendo ya ukatili wa kijinsia”,amesema mmoja wa wanafunzi hao.

Wakizungumzia kuhusu changamoto zinazowafanya washindwe kutoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia wamesema ni pamoja na uoga, vitisho vya kupigwa, mila za uchawi kukosa elimu ya ukatili wa kijinsia pamoja na wazazi wamekuwa wakimaliza kesi za matukio ya ukatili kifamilia hivyo kuogopa kujiingiza kwenye lawama na kuharibu mahusiano katika jamii.

“Pia kuna imani potofu ya hofu ya kurogwa. Tunaogopa kutoa taarifa kwani mhusika akijua kuwa nimemripoti ataniroga niugue au nife”,ameongeza mmoja wa wanafunzi hao.

“Wanawaowapa mimba watoto wa kike wanafahamika, wamo pia waendesha bodaboda, wachimbaji wa madini lakini tunaogopa kusema kwa hofu ya kufanyiziwa na wahusika. Tunaishukuru TGNP kwa kutupatia mbinu za namna ya kuripoti matukio ya ukatili wa kijinsia, tumepewa mbinu za namna gani tunaweza kutoa taarifa kwa viongozi wa serikali za mitaa, vitup vya taarifa na maarifa, walimu na mamlaka zingine ili kuokoa mabinti walio hatarini kuacha masomo yao au kufanyiwa ukatili wa kijinsia”,ameongeza mwanafunzi mwingine.

Kaimu Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Lunguya Lucas Gombe amesema wanafunzi wa kidato cha nne waliopo sasa ni 117 ingawa waliosajiliwa kidato cha kwanza walikuwa 245 hivyo kumekuwa na mdondoko mkubwa wa wanafunzi unaosababishwa na sababu mbalimbali ikiwemo wazazi kuhama, wanafunzi wanaofeli kukimbia shule pamoja na ndoa na mimba za utotoni.

Mwenyekiti Msaidizi wa kituo cha taarifa na maarifa Lunguya, Irene Nyanza amewataka wanafunzi wanapoona viashiria vya ukatili wa kijinsia watoe taarifa kwenye vituo vya taarifa na maarifa pamoja na mamlaka zingine.

Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Msaada wa Kisheria mkoa wa Shinyanga, John Shija ambaye ni Mratibu wa shughuli zinazofanywa na TGNP Mkoa wa Shinyanga amesema vijana wa kiume wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kuwalinda watoto wa kike hivyo waache kufumbia matukio ya ukatili kwa kutoa taarifa za viashiria vya matukio ya ukatili wa kijinsia.

Afisa Kiongozi wa Programu TGNP, Bi. Joyce Mkina lengo la mdahalo ni kuongeza ushiriki wa vijana/wavulana katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia na mdondoko mkubwa wa wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi na sekondari.

Amesema Mdahalo huo ulilenga kujadili masuala ya ukatili wa kijinsia kwa vijana wa kiume shuleni kwa ajili ya kutoa elimu ya namna gani vijana wa kiume wanaweza kuzuia ukatili wa kijinsia shuleni na ndani ya jamii.
Afisa Kiongozi wa Programu TGNP, Bi. Joyce Mkina akizungumza kwenye Mdahalo kwa vijana wa kiume katika shule ya Sekondari Lunguya iliyopo katika kata ya Lunguya halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga wenye lengo la kujadili namna kuzuia ukatili wa kijinsia shuleni na ndani ya jamii.
Afisa Kiongozi wa Programu TGNP, Bi. Joyce Mkina akizungumza kwenye Mdahalo kwa vijana wa kiume katika shule ya Sekondari Lunguya iliyopo katika kata ya Lunguya halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga wenye lengo la kujadili namna kuzuia ukatili wa kijinsia shuleni na ndani ya jamii.
Afisa Kiongozi wa Programu TGNP, Bi. Joyce Mkina akiongoza Mdahalo kwa vijana wa kiume katika shule ya Sekondari Lunguya iliyopo katika kata ya Lunguya halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga wenye lengo la kujadili namna kuzuia ukatili wa kijinsia shuleni na ndani ya jamii.
Afisa Kiongozi wa Programu TGNP, Bi. Joyce Mkina akizungumza kwenye Mdahalo kwa vijana wa kiume katika shule ya Sekondari Lunguya iliyopo katika kata ya Lunguya halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga wenye lengo la kujadili namna kuzuia ukatili wa kijinsia shuleni na ndani ya jamii.
Afisa Kiongozi wa Programu TGNP, Bi. Joyce Mkina akizungumza kwenye Mdahalo kwa vijana wa kiume katika shule ya Sekondari Lunguya iliyopo katika kata ya Lunguya halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga wenye lengo la kujadili namna kuzuia ukatili wa kijinsia shuleni na ndani ya jamii.
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Msaada wa Kisheria mkoa wa Shinyanga, John Shija ambaye ni Mratibu wa shughuli zinazofanywa na TGNP Mkoa wa Shinyanga akizungumza kwenye Mdahalo kwa vijana wa kiume katika shule ya Sekondari Lunguya iliyopo katika kata ya Lunguya halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga wenye lengo la kujadili namna kuzuia ukatili wa kijinsia shuleni na ndani ya jamii.
Afisa Kiongozi wa Programu TGNP, Bi. Joyce Mkina akijadili jambo na mwanafunzi wakati wa Mdahalo kwa vijana wa kiume katika shule ya Sekondari Lunguya iliyopo katika kata ya Lunguya halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga wenye lengo la kujadili namna kuzuia ukatili wa kijinsia shuleni na ndani ya jamii.
Kaimu Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Lunguya Lucas Gombe akizungumza kwenye Mdahalo kwa vijana wa kiume katika shule ya Sekondari Lunguya iliyopo katika kata ya Lunguya halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga wenye lengo la kujadili namna kuzuia ukatili wa kijinsia shuleni na ndani ya jamii.
Mwanafunzi akichangia hoja kuhusu namna ya kuzuia ukatili wa kijinsia shuleni na ndani ya jamii.

Katibu Msaidizi wa kituo cha taarifa na maarifa Lunguya Meja Masalu akizungumza kwenye mdahalo huo

Gaudencia Macheye kutoka kituo cha taarifa na maarifa Lunguya akizungumza kwenye mdahalo huo

Msaidizi wa Kisheria Hawa Hashim akizungumza kwenye mdahalo huo

Wanafunzi wakifuatilia majadiliano

Wanafunzi wakifuatilia majadiliano
Viongozi mbalimbali wakifuatilia majadiliano
Afisa Kiongozi wa Programu TGNP, Bi. Joyce Mkina akiimba na kucheza na vijana wa kiume katika shule ya Sekondari Lunguya iliyopo katika kata ya Lunguya halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga
Vijana wa kiume katika shule ya Sekondari Lunguya iliyopo katika kata ya Lunguya halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga wakipiga picha ya kumbukumbu
Vijana wa kiume katika shule ya Sekondari Lunguya iliyopo katika kata ya Lunguya halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga wakipiga picha ya kumbukumbu na Afisa Kiongozi wa Programu TGNP, Bi. Joyce Mkina (kulia) na Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Msaada wa Kisheria mkoa wa Shinyanga, John Shija ambaye ni Mratibu wa shughuli zinazofanywa na TGNP Mkoa wa Shinyanga (kushoto).

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post