Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Khamis Issah
Mwanamke mmoja mkazi wa Njombe, amejinyonga baaada ya kujifungua mtoto mwenye ulemavu, ambapo Kamanda wa Polisi mkoani humo Khamis Issah, akawasihi wanawake kuwa na huruma na watoto na kuhoji kama mzazi amejinyonga mtoto aliyemuacha atalelewa na nani.
Kamanda Issah ameongeza kuwa kama kuna mtu ana mpango wa kujinyonga basi haina haja ya yeye kushika ujauzito na kisha kujinyonga na kuacha mtoto, na kuwasihi wazazi kujilinda kwa ajili ya watoto wao.
"Wewe unayejinyonga na una watoto, unajinyonga kwa sababu gani, watoto bado wadogo watamtegemea nani, kama wewe una mawazo ya kujinyonga basi usiwatafute hao watoto wewe ujinyonge peke yako, kama wewe usingewatafuta wasingekuwa na wazazi," amesema ACP Issah ajinyonga
Chanzo - EATV
Social Plugin