Na Fadhili Abdallah - Malunde 1 blog Kigoma
Kamanda wa polisi mkoa Kigoma,James Manyama alisema hayo akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mjini Kigoma ambapo alisema kuwa watu hao walikamatwa mwanzoni mwa wiki hii Kijiji cha Kanyonza wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma baada ya kuzuia katika kuzuizi cha polisi Kihomoka.
Kamanda Manyama alisema kuwa awali watu watatu walikamatwa katika kuzuizi hicho cha polisi wakiwa kwenye gari yenye namba za usajili T 948 DQU aina ya Pro Box (mchomoko) wakielekea Mwanza kwenye kijiji cha Nyahunge ambako walikuwa wakipeleka kwa mteja aliyekuwa akihitaji viungo hivyo.
Alisema kuwa baada ya kuwahoji watuhumiwa waliwataja waliokuwa wakipelekewa viungo hivyo wakazi wa Mwanza ambao ni wenyeji wa Kigoma sambamba na watu waliowapa viungo hivyo kutoka wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma ambapo jumla ya watu wote waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo wamefikia tisa.
“Kwa sasa tunafanya uchunguzi zaidi na kuwahoji watuhumiwa kujua kama viungo hivyo vimefukuliwa kwenye kaburi gani na ni mwili wa nani au kuna mtu aliuawa na viungo vyake kuchukuliwa, viungo vilivyopo ni sehemu ya mbavu na mguu mmoja,”alisema kamanda huyo wa Polisi mkoa Kigoma.