Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema takribani askari Polisi wanafunzi 156 wamefukuzwa mafunzo ya kijeshi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo za utovu wa nidhamu na kufanya mambo ambayo hayakubaliki ndani ya shule ya Polisi.
IGP Sirro amesema hayo leo wakati alipofanya ziara kwenye uwanja wa medani za kivita wilaya ya Siha, West Kilimanjaro katika Shule ya Polisi Tanzania, ambapo pia amewaelekeza wanafunzi hao wa kozi ya awali ya askari Polisi kufuata sheria, kanuni na taratibu za shule hiyo ikiwa ni pamoja na kudumisha nidhamu ndani ya Jeshi la Polisi.