Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KATAMBI AWATAKA VIJANA KUTUMIA MUDA WAO KUZALISHA BADALA YA KUWEKA AKILI ZAO KWENYE MAJUNGU NA UCHONGANISHI

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Patrobas Katambi Vijana nchini wametakiwa kutumia muda wao kwa ajili ya kuzalisha badala ya kuweka akili zao kwenye majungu na uchonganishi.

Wito huo umetolewa leo Jumamosi Juni 4, 2022 na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Patrobas Katambi alipozungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma.

Katambi amesema kuna vijana bila kujali kama muda unawapita wao wanatumia muda huo kuzungumzia mafanikio na changamoto za wengine badala ya kutumia muda huo kuzalisha kwa faida ya nchi yao.

Amewahimiza vijana kufanya kazi zaidi na kuwa na uthubutu kwa wanachokiamini bila kusubiri mjomba ambaye hawamjui lini atakuja kuwasaidia.
 
SOMA ZAIDI HAPA CHANZO MWANANCHI.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com