Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi (wa tatu kushoto) akitoa miaelekezo kwa Mwakilishi wa moja ya kampuni za watoa huduma za mawasiliano wakati wa ziara yake na ujumbe wa viongozi wa taasisi za mawasiliano katika kijiji cha Msomero kilichopo Wilaya ya Handeni, Tanga eneo la makazi mapya ya wakazi wanaohamia kutoka Hifadhi ya Ngorongoro. Pamoja nae ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mheshimiwa Siriel Mchembe (wa pili kushoto), Meneja wa Ofisi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)-Kanda ya Kaskazini Mhandisi Imelda Salum (wa kwanza kulia), na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Jabiri Bakari (wa pili kulia). Picha: TCRA.
Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi (wa kwanza kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Ofisi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Kaskazini Mhandisi Imelda Salum kuhusu maendeleo ya uwekaji mnara wa mawasiliano katika kijiji cha Msomero kilichopo Wilaya ya Handeni, Tanga. Mradi huo unatekelezwa na Shirika la Mawasiliano (TTCL). Wengine pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Siriel Mchembe (wa pili kutoka kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari (wa tatu kutoka kushoto), Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Bi. Justina Mashiba (wa nne kutoka kushoto) na Meneja wa TTCL, Tanga Humphrey Ngowi (wa sita kutoka kushoto). Picha: TCRA