Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro
**
Majambazi watatu wameuawa baada ya kupambana na Jeshi la Polisi wakiwa katika harakati za kutaka kupora katika duka, eneo la Goba Dar es Salaam, pambano ambalo lilipelekea askari mmoja kujeruhiwa.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, amesema katika majambazi hao waliouawa wawili wametambuliwa kuwa ni Ridhiwani Sunna Mgeni, aliyewahi kushtakiwa kwa kesi ya mauaji PI 148/2006 na Rajabu Ramadhani aliyewahi kushtakiwa kwa mauaji PI 28/2014.
Taarifa imeeleza kuwa tukio hilo limetokea leo Juni 24, 2022, majira ya saa 6:45 mchana eneo la Goba Tegeta A, wilaya ya Ubungo kwenye duka la miamala ya kifedha lililofahamika kama Skymart Mini supermarket, kundi la majambazi wanne wakiwa na pikipiki aina ya TVS walifika eneo hilo kwa lengo la kuvamia na kupora fedha katika duka hilo.
Kamanda Mambosasa ameeleza kuwa majambazi nao walishambuliwa na kujeruhiwa vibaya, ambapo walipelekwa haraka hospitali lakini kwa bahati mbaya watatu wamepoteza maisha na mmoja alitoroka.
Chanzo - EATV
Social Plugin