Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA VIFO VYA WATU 19 AJALI YA COASTER NA LORI IRINGA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Queen Sendiga kutokana na vifo vya watu 19 katika ajali ya barabarani.

Aidha, Rais Samia amevitaka vyombo vyote vinavyosimamia usalama barabarani kuendelea kutoa elimu kwa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani.

Rais Samia pia anawapa pole wafiwa wote na anaungana na familia hizo katika kipindi hiki kigumu cha majonzi

Aiali hiyo imetokea alfajiri ya leo Alhamisi Juni 10, 2022 katika Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa na kusababisha vifo vya wanaume 14, wanawake 4 na mtoto mmoja wa kike.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Allan Bukumbi, basi dogo la abiria aina ya Coaster lililokuwa likisafiri kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Iringa liligonga lori lililokuwa limeharibika katika eneo hilo.

Wakati majeruhi wakiwa wanaokolewa lilitokea lori lingine lililopoteza muelekeo na kugonga tena Coaster hiyo pamoja na majeruhi waliokuwa wanaokolewa.


ACP Bukumbi amesema Jeshi la Polisi mkoani humo linaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com