Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RC GABRIEL AWATAKA WAFANYABIASHARA MWANZA KUTUMIA FURSA ZA KIBENKI



Na Mwandishi wetu - Mwanza.


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel amewataka wafanyabiashara wa Mwanza kutumia vizuri fursa mbalimbali wanazopewa na banki ya NBC kwani zina manufaa makubwa kwenye kukuza biashara Nchini.


"Benki ya NBC ni benki kongwe na ya serikali ambayo kimsingi inatoa huduma mbalimbali za kibiashara, hivyo wafanyabishara wa Mwanza wajitokeze kuchangamkia fursa zinazopatikana kwenye banki ya NBC", alisema Mhandisi Gabriel.


Vile vile Gabriel alitoa wito kwa benki ya NBC kujikita kwenye kutoa elimu kwa umma ili jamii ielewe umuhimu wa kuweka akiba katika maisha na uwekezaji kwani jambo hilo ni muhimu sana.


Mkurugenzi wa idara ya wafanyabiashara wakubwa NBC makao makuu James Meitaron alisema benki ya NBC ina huduma mbalimbali za ukopeshaji bila dhamana ikiwemo wale waliopata tenda toka Serikalini za kutekeleza miradi ya kimaendeleo kama ujenzi wa barabara.


Pia alieleza kuwa, NBC wamekuwa wabia wa maendeleo ndio maana wanadhamini ligi kuu ya NBC na mambo mengine.


Bwana metro akisema kuwa kwa upande wa wafanyabiashara wadogo nao inawajali kwani kuna huduma maalumu za mikopo kwa wafanyabiashara wadogo na wakati.


Meneja wa NBC Mwanza Thomas Lijaji alisema kuwa, benki ya NBC ina malengo makubwa ya kuwafikia watanzania wengi ili waweze kunufaika na fursa za NBC


Benki ya NBC iliandaa hafla ya jioni kwa wateja wake wote wa Mkoa wa Mwanza ikiwa na lengo la kuwashukuru wateja wake na pia kueleza fursa mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo.


























Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com