Maafisa wa polisi jijini Nairobi wameanzisha msako wa kumtafuta mwanaume anayeshukiwa kusababisha kifo cha mpenzi wake mwenye umri wa miaka 32 baada ya kumsukuma kutoka ghorofa ya tano ya makazi.
Kisa hicho kilitokea katika mtaa wa mabanda wa Mathare jijini Nairobi asubuhi ya Alhamisi, Juni 9,2022.
Kulingana na polisi, mwendazake alikuwa ameenda kumuona mpenziwe Peter Kamau nyumbani kwake wakati ugomvi ulipozuka kati yao.
Mapigano yanasemekana kuzuka kabla ya mshukiwa kumsukuma chini; wapangaji waliwaambia polisi kwamba walisikia kishindo na baadaye kupata mwili wa mwanamke huyo ukiwa kwenye dimbwi la damu, na fuvu lake likiwa limevunjika.
“Marehemu alikuwa alikutana na Kuria nyumbani kwake Alhamisi asubuhi kabla ya ghasia kutokea.
"Alifunga nyumba yake na kwenda kujificha. Tunaomba yeyote aliye na taarifa zinazoweza kupelekea kukamatwa kwake au apige ripoti katika kituo cha polisi kilicho karibu," mkuu wa polisi wa Nairobi James Mugera alinukuliwa na Nation akisema.
Mtuhumiwa alihepa mara moja katika eneo la tukio; polisi waliondoka eneo la tukio wakiwa na walinzi waliokuwa wakisimamia jengo hilo kwa mahojiano kabla ya kuwaachilia baadaye.
Mwili wa mwanamke huyo kwa sasa upo katika makafani ya City, Nairobi, ukisubiri upasuaji.
Chanzo - Tuko News
Social Plugin