Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ATUPWA JELA MIAKA 30 KWA KUBAKA MTOTO WAKE WA KUMZAA WA MIAKA 6


Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemhukumu kifungo cha miaka 30 na fidia ya Tsh. Milioni moja Kumbuka Mhotelwa (30) mkazi wa Kitwiru wilaya ya Iringa kwa kosa la kumbaka Mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 6.


Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mwandamizi Emmy Msangalufu aamesema Mtuhumiwa amekutwa na hatia ya kutenda kosa hilo tareh 19/11/2020 ambapo alikuwa akiishi na Mke wake ambaye alikuwa mgonjwa na alikuwa na kawaida ya kushtuka usiku ili kuweza kunywa maji.

Anasema siku ya tukio alishtuka usiku na kukuta Mumewe hayupo kitandani na alipotazama sebuleni akamuona Mumewe akiwa anambaka Mwanae aliyekuwa na umri wa miaka 6 huku pembeni yake kukiwa na Mtoto mwingine mwenye umri wa miaka mitatu na alikuwa macho akishuhudia Baba yake akimbaka Dada yake.

Baada ya kushuhudia hivyo alipiga kelele kumkataza Mumewe asiendelee na tukio hilo lakini haikusaidia kwa sababu Mke alikuwa hawezi kusimama na hivyo kushindwa kumzuia kuendelea kubaka, baada ya kumaliza Tukio hilo Mtuhumiwa alimtisha Mke wake kuwa endapo atasema popote baasi atamuua.

Hata hivyo baada ya kupambazuka Mkewe alikwenda kutoa taarifa katika kituo cha Polisi ndipo Mtuhumiwa akakamatwa na Mtoto akapelekwa hospitalini walipothibitisha kuwa Mtoto huyo alikuwa amebakwa kutokana na kuwa na michubuko.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com