Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JAMII YATAKIWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KWENYE UJENZI WA VYOO BORA ILI KULINDA NA KUDUMISHA AFYA ZAO

Afisa Afya Mkoa wa Kagera Bw. Zabron Segeru

Na Mbuke Shilagi Kagera.


Jamii imetakiwa kushiriki kikamilifu kwenye ujenzi wa vyoo bora ili kulinda na kudumisha afya zao.


Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake Juni 21,2022, Afisa Afya Mkoa wa Kagera Bw. Zabron Segeru amesema kuwa ili mpango wa vyoo bora kutimia jamii nayo inatakiwa kushiriki kikamilifu kupitia mikutano ya Serikali za mitaa ili kufahamu umuhimu na faida za vyoo bora.


Bw. Segeru ameongeza kuwa wanaimarisha vyoo bora na kila kaya kuwa na vyoo bora katika Mkoa ili kuepukana na magonjwa ambayo yanakuwa yanatokana na kutokuwa na vyoo bora.


"Kama watu watatumia vyoo bora, watakuwa na afya njema hivyo itakuwepo nguvu kazi katika Mkoa" Amesema.


Amewataka viongozi wa Serikali za mitaa kushirikiana na idara ya Afya kuanzia ngazi ya mtaa mpaka Mkoa ili kuhakikisha elimu inapotolewa kwa wananchi na viongozi nao washiriki ili kuhamasisha jamii.


"Pia nitumie fursa hii kuwaomba wadau mbalimbali waendelee kujitokeza ili kuwawezesha wananchi hasa kaya masikini ambazo hazina uwezo wa kujenga vyoo bora kuweza kuwajengea kwani hiyo itatufanya tufikie malengo ya asilimia 100", amesema Segeru.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com