Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HILI NDIYO KABILA AMBALO UKITAKA KUOA AU KUTOA TALAKA LAZIMA UKATWE VIDOLE


Mwanaume kabila la Dani akiwa amekatwa vidole

ACHANA na stori za uongo kuhusu biashara ya vidole vya miguu nchini Zimbabwe, huko Papua Guinea kuna kabila linaitwa Dani (Dani tribe) ambalo mwanaume anapotaka kuoa, sharti akate kidole chake cha mkono wa kulia na kumpelekea mkewe mtarajiwa kama sehemu ya mahari na upendo wake wa dhati kwake.
Utamaduni wa watu wa Dani wanaoishi nchini Guinea

Kwa mujibu wa Wikipedia, katika kabila hilo, kama mwanaume anataka kumpa talaka mkewe, pia ni sharti akate vidole vyake viwili vya mkono wa kushoto kama takwa la talaka.
watu wa Papua Guinea wanaheshimu mila na desturi zao

Na kama mume akifa, mkewe ni sharti akate vidole vyake vyote vya mikono kama ishara ya upendo na uaminifu na kiapo kwake kuwa hataolewa na mwanaume mwingine tena baada ya mumewe kufa.

Kifupi, kwenye kabila hili mtu anapooa, anapotoa talaka au anapokufa, lazima kuna vidole vitakatwa.
Cc; @sifaelpaul

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com