Watu 19 wamefariki dunia na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi dogo aina ya Costa na lori la mizigo karibu na eneo la Changarawe, Mafinga mkoani Iringa leo Juni 10, 2022.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa (RPC), Allan Bukumbi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akisema idadi kamili ya majeruhi na taarifa nyingine zitatolewa baadae.
"Ni kweli ajali hiyo imetokea na vifo ni 19, kuhusu majeruhi ntakupa idadi kamili nikifika eneo la tukio maana ndio naenda nilikuwa safarini kidogo" ameeleza RPC Bukumbi
Social Plugin