Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

INTERNEWS, MPC ZAWANOA WAANDISHI WA HABARI MWANZA


Na Chausiku Said - Mwanza

Waandishi wa habari Mkoani Mwanza wametakiwa kuandika habari zitakazoleta tija katika jamii na kuacha kujiingiza kwenye mitego ya kuandika habari za upotoshaji.


Rai hiyo umetolewa leo na Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo wakati akifungua mafunzo ya waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza yaliyoandaliwa na Shirika la Internews kwa kushirikiana na USAID yenye lengo la kuwakumbusha waandishi jukumu la kusoma maadili ya uandishi wa habari na sheria na taratibu kama zilivyoainishwa kwenye sheria ya vyombo vya habari ya mwaka 2016.


Mihayo ameleeza kuwa mafunzo hayo yatawasaidia waandishi wa habari kuhakikisha wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa.


Amesema kuwa sekta ya habari imezidi kupamba moto hasa kwa waandishi wa habari za mtandaoni kitendo ambacho hupelekea wengi kutumbukia kwenye mitego ya uandishi wa kupotosha hivyo ni lazima kuwaepusha waandishi kwenye dimbwi hilo.


Aidha ameleeza kuwa kumekuwa waandishi wa na wamiliki wa blogs wanapaswa kuandika habari ambazo maudhui ya ndani na nje yanaendana.


" Mimi kuna siku nilimpigia mwandishi mmoja baadae ya kuona alichokiandika kwenye blog yake kama kichwa cha habari hakiendani na nilichoka ndani akanijibu kuwa anatafuta watazamaji", alisema Mihayo.


Mihayo amesema kuwa baada ya serikali kufungulia Uhuru wa vyombo vya habari waandishi waandishi wengine wanasajli TV zao na Blog Kwa gharama nafuu ya sh 500,000 baada ya kupewa usajili hivyo hupelekea kuweka habari zisizo sahihi.


Kwa upande wake Wwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza Edwin Soko amesema kuwa waandishi wanatakiwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kitaaluma na miiko ya uandishi wa habari.

"Tunatamani kuona waandishi wa habari wakifanya kazi zao bila kuvunja sheria wala kukumbwa kwenye mkondo wa sheria lakini pia waweze kubaini habari zisizo sahihi na kuziepuka.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com