Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

OJADACT YAADHIMISHA SIKU YA OPEN DATA DAY KWA KUWANOA WAANDISHI WA HABARI...YAHAMASISHA WANAHABARI KUTUMIA TAKWIMU KULINDA MAZINGIRA

Na Mwandishi wetu - Mwanza

Chama cha Waandishi wa habari wa kupiga vita Matumizi ya Dawa za Kulevya Tanzania leo kimeadhimisha siku ya Open Data kwa kwa Mwaka 2022 kwa kuwapa mafunzo waandishi wa habari wa Mwanza.


Akifungua maadhimisho hayo Mwenyekiti wa OJADACT Bwana Edwin Soko amesema maadhimisho hayo yanalenga kutumia takwimu kwenye utunzaji wa fukwe Tanzania.


" Ndugu zangu waandishi wa habari tumieni takwimu kwenye kuandika habari juu ya uvumilivu wa fukwe kwani kauli mbiu ya Mwaka huu ni uwazi wa takwimu kwenye kuimarisha maisha ya yote", alisema Mwenyekiti Soko.


Nae Mratibu wa OJADACT Lucyphine Kilanga alisema kuwa, kwa sasa kumekuwa na mabadiliko makubwa ya tabia Nchi yanayopelekea uharibifu wa fukwe.


Kilanga alisema waandishi wa habari wana nafasi kubwa ya kuandika habari za umuhimu wa kutumia data kwenye kulinda mazingira.


Maadhimisho ya Open Data Day 2022 yameandaliwa na OJADACT kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Open Knowledge Foundation 
Mafunzo hayo yamejumuisha zaidi ya wanaandishi wa habari thelathini toka vyombo vya habari mbalimbali Mkoa wa Mwanza.
Mwenyekiti wa OJADACT, Edwin Soko (kulia) akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Mratibu OJADACT, Lucyphine Kilanga akizungumza
Mratibu OJADACT, Lucy Kilanga.
Mwanahabari Glory Kiwia (kulia) akichangia hoja kwenye maadhimisho hayo.
Waandishi wa Habari jijini Mwanza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com