Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano- LGTI akiwaelekeza baadhi ya wanafunzi waliomaliza elimu ya Sekondari waliotembelea kwenye banda la maonyesho la chuo hicho kuhusu namna ya kujiunga na chuo hicho ikiwa ni moja ya nguzo muhimu katika kuwajenga,kuwaimarisha na kuwapa ari ya kujiendeleza katika kozi mbalimbali.
Na Dotto Kwilasa,DODOMA
CHUO
cha Serikali za Mitaa (LGTI),Hombolo-Dodoma kimesema kina mpango wa
kutembelea shule za Sekondari nchi nzima kuona namna ya kuwaelimisha
wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne na kushindwa kupata alama za
kujiunga na kidato cha tano kutokata tamaa na badala
yake kutakiwa kujiunga na chuo hicho kwa mpango maalumu wa kujiendeleza katika kozi mbalimbali.
Afisa
Udahili wa Chuo hicho Misu Chibona amesema hayo leo katika Maonesho
ya Elimu ya Sayansi na mafunzo ya ufundi stadi (TVET) yanayoendelea
Jijini hapa yenye lengo la kuhasisha wanafunzi kujiunga na vyuo vya
ufundi vya kati na kueleza kuwa mpango huo utasaidia kwa kiasi kikubwa
kuwaandaa wanafunzi hao katika malengo ya maendeleo endelevu na kuachana
na utegemezi.
Amesema,kumekuwa
na tabia ya baadhi ya wazazi kuwavunja moyo watoto wao pale wanapo ona
wameshindwa mitihani na hawawezi kuendelea na masomo kutokana na alama
zao kuwa ndogo na kueleza kuwa Kila tatizo linapotokea wazizi na walezi
hawapaswi kuwavunja moyo bali wanapaswa kutafuta mbinu mbadala za
kukabiliana na tatizo lililopo.
Pamoja
na hayo amewataka wazazi wenye watoto wanaomaliza kidato cha nne kuacha
kuwakatisha tamaa wanapohitimu na kupata alama zisizoruhusu kuingia
kidato cha tano bali wawapeleke chuoni hapo kujiunga na kozi
zinazoendana na alama zao.
Amefafanua
kuwa kutokana na kuona matukio mengi mabaya yanayofanywa na watoto
waliokatishwa tamaa na alama zao za mitihani LGTI kimeona kuna haja ya
kutembelea mashuleni kuhamasisha wanafunzi kutojisikia vibaya wanapopata
alama hizo bali waangalie njia nyingine ya kujiendeleza .
"Kwa
kuanza tayari tumetembelea Shule zote za Sekondari katika Jiji la
Dodoma na kueleza kozi tunazotoa lakini pia tuliwaambia sisi tunapokea
hata mwanafunzi aliyefaulu kwa alama angalau D nne ili kusoma ngazi ya
cheti na kisha kuendelea na ngazi nyingine,"alisema Chibona.
Kwa
upande wake Mhadhiri mwandamizi wa chuo hicho Bundala Dodo ametumia
nafasi hiyo kutaja kozi zinazoruhusu mwanafunzi aliyefaulu kwa alama ya D
nne kuwa ni utawala katika Serikali za Mitaa,Uhasibu na fedha,Maendeleo
ya jamii,Kumbukumbu na nyaraka,Rasilimali watu na manunuzi.
Amesema,"tunataka
kuokoa jamii na mwelekeo wake hususani wanafunzi wa sekondari
walioshindwa kupata alama za kujiunga na elimu ya juu wasijione wakosefu
wanapopata alama zisizoruhusu kuingia kidato cha tano Chuo chetu tuna
kozi za kuwapeleka juu,"amesema
Ameongeza kuwa
baadhi ya wazazi wamekua mstari wa mbele kuwarudisha nyuma watoto
katika kipengele cha elimu kwa kuwakatisha tamaa kwamba wakisoma ngazi
ya cheti elimu yao itakuwa ndogo kitendo ambacho siyo kweli kwani
mwanafunzi wao akimaliza ngazi ya cheti anauwezo wa kuendelea kupata
Diploma na kuendelea zaidi hadi degree.
"Nawasisitiza
wazazi mtoto akishindwa kuchaguliwa mpeleke akapate elimu inayoendana
na alama zake kwasababu anayoendelea ndivyo elimu yake
inavyokuwa,niwaambie wanafunzi ukisoma chuo chetu kinafaida kwasababu
Serikali imetoa nafasi za ajira katika mikoa mbalimbali za watendaji wa
vijiji na kata hivyo wanafunzi wakihitimu ajira zipo,"amesema.
Social Plugin