Tukio hilo la aina yake limetokea leo Jumapili Juni 5 Mwaka huu, ambapo lengo kuu la kumuita mganga huyo, ilikuwa ni kuwarudisha watu waliomuiba magodoro mawili,,Radio aina ya Subwoofer,Viazi mviringo kg 20 na sufuria iliyokuwa na nyama ya ng'ombe iliyopikwa.
Wizi katika mji huo umekithiri kwa matukio ya watu mbalimbali kuibiwa vitu mbalimbali wakiwemo na kuku kwa kuvunja madirisha na milango kwenye nyumba nyakati za usiku na mchana.
Imeelezwa kuwa mara baada ya dawa hiyo kufanyika ambapo mhusika,Mantesa Lukumba ambaye ni mkazi wa Maswa alileta mganga ili kuwabaini wahusika na kuwashirikisha watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa kitongoji wa Majengo mahali anapoishi.
Hivyo kila mmoja wakiwemo vijana hao waliombwa kunywa dawa ya mganga huyo au kuacha maana ni hiyari hivyo watu walio wengi waliamua kunywa na vijana hao walirudi na kuanza kukata majani na kuyala kama wafanyavyo Ng'ombe,kula mchanga na takataka kitendo ambacho wamekifanya wakiwa kwenye hali ya kutojitambua, huku wakishuhudiwa na Umati wa watu waliokusanyika kwenye nyumba hiyo.
Baadaye askari polisi walifika majira ya saa 1:40 jioni na kuwachukua na kuwapeleka kituo cha polisi kwa ajili ya usalama wao lakini imeelezwa kuwa hadi watakaporejesha kiasi cha fedha kila mmoja Sh 800,000 kufidia gharama za thamani ya vitu walivyoiba ndipo watakaporudishwa kwenye hali yao ya kawaida.
Kwa upande wake aliyeibiwa Mantesa , ameeleza ni kwa namna gani alibaini kuwa ameibiwa alisema kuwa wezi hao waliruka ukuta usiku wakiwa wamelala wakavunja dirisha na kukata nondo na kufanikiwa kuiba vitu hivyo ambavyo hadi sasa havijapatikana kwahiyo msaada mbadala ndiyo tulioutumia na ndiyo hiki mnachokiona.
Tazama video hapa
Tazama Wezi wakila majani kama wanyama Maswa