Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ALIYEANDIKA KITABU CHA JINSI YA KUUA MME WAKO ATUPWA JELA MAISHA


Nancy Crampton Brophy, aliyehukumiwa kifungo cha maisha
****
Mwandishi wa kitabu chenye jina lisemalo 'Jinsi ya kumuua mume wako' kutoka nchini Marekani aitwaye Nancy Crampton Brophy, mwenye umri wa miaka 71 amehukumiwa kifungo cha maisha baada ya kukutwa na hatia ya mauaji ya mume wake aliyoyatekeleza mwaka 2018.

Imeelezwa kwamba tukio la mauaji lilifanyika mahali ambapo mume wake huyo aitwaye Daniel Brophy, alikuwa akifanya kazi kama mpishi na mwili wake ulikutwa sakafuni kwa majeraha ya risasi mbili mnamo Juni 2008.

Nancy Crampton Brophy, alihukumiwa maisha hapo jana Juni 13, 2022, na kwamba hata silaha aliyoitumia haijulikani ilipo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com