MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA SALAMA DUNIANI: TBS YAHIMIZA UZINGATIAJI WA USALAMA WA CHAKULA

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mhandisi Johaness Maganga (katikati) akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Chakula Salama Duniani (World Food Safety Day) yaliyofanyika leo Juni 7,2022 katika ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mhandisi Johaness Maganga akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Chakula Salama Duniani (World Food Safety Day) yaliyofanyika leo Juni 7,2022 katika ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora Shirika la Viwango Tanzania, Bw.Lazaro Msasalaga akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Chakula Salama Duniani (World Food Safety Day) yaliyofanyika leo Juni 7,2022 katika ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam. Mwakilishi kutoka Shirika la Afya la Umoja wa Kimataifa (WHO) Bi.Rose Shija akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Chakula Salama Duniani (World Food Safety Day) yaliyofanyika leo Juni 7,2022 katika ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam. Afisa Afya na Mazingira kutoka Wizara ya Afya (Wizara ya Afya) Bi.Josephine Kapinga akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Chakula Salama Duniani (World Food Safety Day) yaliyofanyika leo Juni 7,2022 katika ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam. Afisa Biashara kutoka Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bw.Denis Mzamily akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Chakula Salama Duniani (World Food Safety Day) yaliyofanyika leo Juni 7,2022 katika ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wadau mbalimbali wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Chakula Salama Duniani (World Food Safety Day) yaliyofanyika leo Juni 7,2022 katika ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

**************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Makadirio yaliyofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) mwaka 2015 yanaonesha kuwa kila mwaka, zaidi ya watu milioni 600 duniani huugua, na watu 420,000 kati yao hufa kutokana na kula chakula kisicho salama. Magonjwa haya hutokea zaidi kwa watu wenye kipato cha chini na zaidi kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.

TBS imeweka mifumo ya kiudhibiti ili kuhakikisha kuwa chakula kilichopo katika soko hapa nchini ni salama ili kuilinda jamii dhidi ya madhara yatokanayo na kula chakula kisicho salama.

Ameyasema hayo leo Juni 7,2022 katika Ofisi za TBs Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mhandisi Johaness Maganga wakati akizungumza na wadau mbalimbali katika kuadhimisha Siku ya Chakula Salama Duniani (World Food Safety Day).

Amesema mara kadhaa TBS imekuwa ikishirikiana na wadau wa chakula ili kufikia lengo la kuwa na chakula salama katika soko, hivyo basi maadhimisho haya yamewashirikisha pia wadau wa usalama wa chakula kutoka wizara na taasisi mbalimbali za serikali na za kimataifa, ikiwemo Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Wizara ya Afya, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Taasisi ya Chakula na Lishe pamoja na Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa Serikali. Vilevile, ofizi za mashirika ya kimataifa, Shirika la Afya la Umoja wa Kimataifa (WHO) pamoja na Shirika la Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) wamejumuika nao katika maadhimisho haya.

"Tunatambua mchango mkubwa kutoka kwa wadau hawa katika kuhakikisha usalama wa chakula nchini, ikiwa ni pamoja na kushiriki katika masuala mbalimbali kama vile kuandaa sera, kanuni na miongazo mbalimbali katika uzalishaji, usafirishaji, uuzaji na uandaaji wa chakula". Amesema Mhandisi Maganga.

Aidha Mhandisi Maganga amesema kutokana na suala la usalama wa chakula kuwa mtambuka, mfumo thabiti wa udhibiti wake unapaswa kuwa shirikishi, ukihusisha afya ya binadamu, wanyama, mimea na mazingira.

"Wanyama na mimea ndio chanzo kikubwa cha chakula cha binadamu. Afya ya wanyama ni muhimu ili kuepuka magonjwa yanayoambukizwa kwa binadamu kwa kula nyama kutoka kwa wanyama hao". Amesema

Pamoja na hayo ameeleza kuwa kuadhimisha Siku ya Chakula Salama Duniani kwa mwaka 2022, TBS imejikita katika kutoa elimu kwa jamii kupitia vyombo mbalimbali vya habari. Mada na matangazo kuhusu usalama na ubora wa chakula zimekuwa zikitolewa katika redio, televisheni, magazeti na mitandao ya kujamii kwa wiki moja, kuanzia tarehe 30 Mei,

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Shirika la Afya la Umoja wa Kimataifa (WHO) Bi.Rose Shija amesema WHO imeongoza juhudi za kutathmini ukubwa wa tatizo la magonjwa yatokanayo na chakula kisicho salama duniani na imesaidia nchi kujenga au kuimarisha mifumo ya kitaifa ya ufuatiliaji wa magonjwa yatokanayo na chakula kisicho salama.

Amesema WHO imehakikisha kuwa viwango vya kimataifa vya usalama wa chakula Codex Alimentarius vinazingatia afya ya Umma na kwamba nchi zilizo na uwezo mdogo zinajengewa uwezo ka kushiriki kwenye mafunzo ya Codex.

"Tunatoa wito kwa wadau wote kukuza na kuendeleza utamaduni wa usalama wa chakula na pia kuzingatia viwango vya chakula vya kimataifa na vya ndani, kukuza utunzaji salama wa chakula pamoja na kutoa elimu ya usalama wa chakula.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post