Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MITANDAO YA KIJAMII YACHANGIA MAPAMBANO DHIDI YA UKATILI


Naibu Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa jamii hicho Kitengo Cha Fedha na Mipango, Profesa Justice Urassa akizungumza wakati wa uwasilishaji wa utafiti mdogo wa kupinga ukatili wa kingono kwenye mitandao ya kijamii uliofanywa na Chuo cha Ustawi wa Jamii, Jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Juni 24, 2022.Naibu Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa jamii hicho Kitengo Cha Fedha na Mipango, Profesa Justice Urassa akizungumza na waandishi wa habari baada ya uwasilishaji wa utafiti mdogo wa kupinga ukatili wa kingono kwenye mitandao ya kijamii uliofanywa na Chuo cha Ustawi wa Jamii, Jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Juni 24, 2022Mtafiti katika Chuo Cha Ustawi wa Jamii Bi.Itika Gwamaka akiwasilisha matokeo ya utafiti mdogo wa kupinga ukatili wa kingono kwenye mitandao ya kijamii uliofanywa na Chuo cha Ustawi wa Jamii, Jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Juni 24, 2022.Mhadhiri kutoka chuo Cha Ustawi wa Jamii Dkt. William Manyama akizungumza wakati wa uwasilishaji wa utafiti mdogo uliofanywa na Chuo cha Ustawi wa Jamii Jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Juni 24,2022Baadhi ya wadau waliojitokeza kusikiliza matokeo ya utafiti mdogo uliofanywa na Chuo cha Ustawi wa Jamii.

******************

Imeelezwa kuwa mitandao ya kijamii ina mchango mkubwa katika kupambana na vitendo vya ukatili kwasababu imechukua nafasi kubwa ya maisha ya watu.

Hayo yamebainishwa leo Juni 24 wakati wa mawasilisho ya matokeo ya utafiti mdogo wa kupinga ukatili wa kingono kwenye mitandao ya kijamii uliofanywa na taasisi ya Ustawi wa jamii kwa lengo la kutanua mawazo ya kukabiliana na vitendo vya ukatili.

Akizungumza wakati wa uwasilishaji wa matokeo ya utafiti huo leo Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Maktaba ya Chuo Cha Ustawi wa Jamii Naibu Mkuu wa Chuo hicho Kitendo Cha Fedha na Mipango Profesa Justice Urassa ametoa wito kwa Vyuo vikuu na vya Kati kufanya Utafiti kwa kutumia njia ya Madodoso na Mahojiano ili kupata Takwimu sahihi za Matukio ya Ukatili wa Kingono kwa Wanafunzi wa Vyuo hivyo na Jamii kwa Ujumla.

Profesa Urassa amesema Utafiti huo wa kutumia Mitandao ya Kijamii Kupinga Ukatili wa Kingono kwa Wanafunzi ni Muhimu kwenye Nchi ya Tanzania kweni kumekuwa na ongezeko na Matukio hayo yanayowapata Wanafunzi wawapi Mashuleni.

"Wanafunzi wanatakiwa kutumia Madawati ya kijinsia yaliyopo vyuoni kupata ushauri Nasaha pale anapotendewa Ukatili wa Kijinsia na kuachana na kutumia Watu ambao hawana Weledi wa Kutoa Ushauri huo Hali inayoweza kusababisha Kushawishika kufanya Vitendo visivyofaa" amesema Profesa Urassa

Naye Mtafiti katika Chuo Cha Ustawi wa Jamii Itika Gwamaka, amesema Utafiti huo umelenga Wanafunzi pamoja na Jamii kwani Vitendo hivyo viko kwenye Jamii Huku Akitoa wito kwa Vyombo vya Habari kuendelea Kupinga Vitendo vya Ukatili wa kijinsia kupitia vipindi mbalimbali na Kutoa Elimu kwa Jamii kuhusu Athari za Vitendo hivyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com