***********
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KLABU ya Simba imefanikiwa kuondoka na alama tatu mara baada ya kumchapa Mtibwa Sugar kwa mabao 2-0 kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mabao yamewekwa na mastaa wao hatari Pape Sakho na lingine likifungwa na Peter Banda na kuiwezesha timu yao kuondoka na alama tatu kwenye mchezo huo.
Licha ya kuwa Simba Sc inacheza kukamilisha ratiba tu lakini imecheza mpira safi ambao ulivutia kwa wengi hasa mashabiki wa timu hiyo.
Mechi hiyo pia ilitumika kwaajili ya kumuaga beki wao kisiki raia wa Ivory Coast Paschal Wawa ambaye anaachana na klabu hiyo baada ya kumalizika kwa mkataba wake na wanasimbazi hao.
Social Plugin