Baadhi ya majengo ya shule ya Sekondari Nkola
Katibu Mkuu wa Kanisa la AICT Tanzania Mchungaji Josephales Mtebe,akizungumza mara baada ya kumaliza kukagua mazingira na miundombinu ya shule ya Nkola sekondari.
Na Mwandishi wetu Shinyanga press club blog
Kanisa la African Inland Church (AICT) Dayosisi ya Shinyanga limefanikiwa kuirejesha shule yake ya Bishop Nkola Sekondari iliyokuwa imepigwa mnada na benki ya CRDB tawi la Shinyanga kutokana na kushindwa kulipa mkopo waliokopa mwaka 2017.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya kufanyika mazungumzo baina ya benki ya CRDB na uongozi wa Dayosisi ya Shinyanga pamoja na mfanyabiashara Philemon Mushi aliyenunua shule hiyo kupitia mnada wa hadhara uliofanyika mwaka 2017 baada ya kushinda na kukidhi vigezo.
Akizungumza na baadhi ya waumini na Viongozi wa Kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Katibu Mkuu wa Kanisa la AICT Tanzania Mchungaji Josephales Mtebe amesema haikuwa rahisi kuirejesha shule hiyo mikononi mwao ila kwa uwezo wa Mungu wamefanikiwa kuirejesha.
Katibu Mkuu Mch. Mtebe amesema wamekamilisha taratibu zote ikiwemo kulipa fedha walizokuwa wakidaiwa na benki ya CRDB pamoja na fidia kwa mfanyabiashara aliyekuwa ameinunua shule hiyo kupitia mnada wa hadhara wa benki ya CRDB.
“Kila mtu alikata tamaa ya kuendelea mbele lakini tunamshukuru mungu kwa kufikia hatua nzuri kwa kushirikiana na benki ,pia nimshukuru Mushi kwa kukubali na niwashukuru waumini kwa kujitoa kuchangia fedha zao ili kulipa deni tulilokuwa tunadaiwa na benk ya CRDB baada ya kushindwa kurejesha mkopo”amesema Katibu Mkuu Kanisa la AICT Tanzania.
Amesema kilichofanywa na benki ya CRDB kilikuwa kwenye utaratibu wake kwani wao walishindwa kurejesha fedha walizokuwa wamekopa ,jambo ambalo lilisababishwa na baadhi ya watu ndani ya Kanisa waliokuwa wamepewa dhamana ya kusimamia.
Amewataka waumini kuwa na ushirikiano na kuacha kunyosheana vidole kwani ni wakati wa kujenga umoja wao na kuangalia namna ya kuiendeleza shule yao ya Bishop Nkola ili kuleta tija zaidi kwani tayari deni la zaidi ya Shilingi milioni miatatu walilokuwa wanadaiwa wamelipa.
Kwa upande wake Askofu Mkuu msaidizi wa Kanisa la AICT Tanzania ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Shinyanga Zakayo Bugota amesema ushirikiano pekee ndiyo utakaosaidia kuendeleza umoja wao na kumuomba mungu awawezeshe kuiendeleza taasisi hiyo ya elimu.
Naye mfanyabiashara Philemon Mushi aliyekuwa amenunua shule hiyo,amesema yeye aliuziwa na benki ya CRDB kwa kufuata sheria zote, hivyo hata asingenunua yeye wangenunua watu wengine na ameamua kukubali kurudisha shule hiyo kwa Kanisa ili waishi kwa amani.
Viongozi wa Kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga na baadhi ya waumini wakikagua maeneo ya shule ya Sekondari Nkola iliyokuwa imepigwa mnada na benki ya CRDB ambayo kwa sasa imerejeshwa na kanisa hilo.
Ukaguzi unaendelea
Baadhi ya majengo ya shule
Askofu wa Kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Askofu Zakayo Bugota akiwa na baadhi ya waumini.
Ukaguzi unaendelea
Majengo ya shule
Ukaguzi unaendelea
Baadhi ya viongozi wa AICT wakiangalia maeneo ya shule
Aliyevaa shati jeupe na kofia ni Philemon Mushi mfanyabiashara aliyekuwa amenunua shule hiyo kupitia mnada.
Viongozi wakikagua mazingira ya shule
Mfanyabiashara Philemon Mushi aliyekuwa amenunua shule ya Nkola sekondari
Baadhi ya waumini na viongozi wa dini.
Askofu wa Kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Askofu Zakayo Bugota akiomba mara baada ya kukagua shule.
Maombi yakiendelea
Social Plugin