KLABU ya soka ya Simba imetngaza kuachana na mchezaji wao raia wa Ivory Coast Pascal Wawa ambaye amehudumu ndani ya kikosi hicho kwa muda wa misimu minne akiisaidia Simba SC kushinda makombe ya Ligi Kuu pamoja na makombe ya FA na pia kushiriki vizuri kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.
Kupitia mtandao wa Instagram wa Klabu hiyo Simba imemshukuru Pascal Wawa kwa mchango wake kwenye mafanikio ya klabu hiyo.
“Asante Pascal Wawa baada ya kutumikia timu yetu kwa miaka minne, Pscal Wawa hatakuwa sehemu ya kikosi chetu cha msimu ujao.
Mkataba wake utamalizika mwisho wa mwezi huu na mchezo wa alhamisi dhidi ya Mtibwa Sugar utakuwa mchezo wake wa mwisho.”
Simba SC inaendelea na taratibu za usajili ambapo tayari baadhi ya nyota wa kimataifa wameanza kuondoka klabuni hapo akiwemo kiungo mshambuliaji raia wa Zambia Rally Mbwalya aliyetimkia katika kikosi cha Amazulu cha nchini Afrika Kusini.
Aidha timu hiyo tayari imeshafanikiwa kuinasa saini ya nyota wa Zanaco na timu ya Taifa ya Zambia Moses Phiri huku majina ya wachezaji kama Habib Kyombo, Victor Akpan pamoja na nyota wengine wa kimataifa yakiendelea kuhusishwa kujiunga na klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya msimbazi, Kariakoo jijini Dar es Salaam
Social Plugin