TFRA YAANZISHA MFUMO WA KIELEKTONIKI KURAHISISHA HUDUMA KWA WATEJA WA MBOLEA

 

 

Kaimu Meneja wa TEHAMA na Takwimu Maafisa kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania –TFRA Salehe Kejo akizungumza katika banda lao kwenye Maonyesho ya 46 ya kimataifa ya Biashara Sabasaba akielezea kuhusu  mfumo wa Kielektoniki wa Mbolea.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano,Mawasiliano na Elimu kwa Umma TFRA Matilda Kasanga akizungumza kuhusu ushiriki wao katika Maonyesho ya 46 ya kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es salaam.

Moja ya mwananchi aliyetembelea katika Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania –TFRA kwenye Maonyesho ya 46 ya kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es salaam.

Picha ya pamoja ya Maafisa kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania –TFRA wakiwa katika banda la kwenye Maonyesho ya 46 ya kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es salaam.(picha na Mussa Khalid)

.......................

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania -TFRA imeanzisha mfumo wa Kielektoniki wa Mbolea ili kuboresha utoaji wa huduma za Mamlaka hiyo kwa njia ya mtandao na kurahisisha huduma kwa wateja.

Akizungumza jijini Dar es salaam katika Maonyesho ya 46 ya kimataifa ya Biashara Sabasaba Kaimu Meneja wa TEHAMA na Takwimu TFRA Salehe Kejo amesema mfumo huo umekuwa na mafanikio kwa kuwa utoaji huduma umeimarika.

Kejo amesema kuwa mafanikio ya mfumo huo ni umesaidia huduma kufanyika kwa wakati ikiwemo utoaji wa leseni ndani ya muda mfupi pamoja na usajili wa mbolea kwa muda mchache tofauti na ilivyokuwa awali.

‘Mfumo huu ni katika kuboresha baadhi ya huduma za Mamlaka kwa kuwa huduma zetu zote zinapatikana katika mtandao wateja waliokuwa wanaokuja kwenye mamlaka kufuatilia leseni zao sasa hivi wanapata kwa njia ya mtandao’amesema Kejo

Aidha Kejo amesema tangu mfumo huo uanze kutumika wamewasajili wafanyabiashara 3800 na kwa mwaka huu fedha unaomalizika wamewsajili wafanyabiashara 2200 hivyo amewasisitiza wananchi kuendelea kutumia huduma hiyo ya kielekroniki ili kupata huduma kwa wakati.

Amesema mfumo huo unapatikana masaa 24 kwa siku saba za wiki ambapo huduma hiyo ukifanya kwa muda wakazi ndani ya lisaa limoja unaweza kupata leseni.

Hata hivyo Mamlaka hiyo imewataka watanzania kuendelea kujitokeza kwa wingi katika banda lao lililopo katika Maonyesho ya sabasaba ili waweze kujifunza na kupata uelewa wa masuala mbalimbali kuhusu matumizi ya mbolea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post