Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari-Tanzania, Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb.) (Kulia) akifuatana na Katibu Mkuu Dkt. Jim Yonazi (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari (katikati-nyuma) walipowasili Rwanda Convention Centre jijini Kigali, Rwanda kushiriki Mkutano Mkuu wa Maendeleo ya Mawasiliano Duniani (ITU-WTDC-2022) ulioandaliwa na Shirika la Mawasiliano Duniani-ITU. Waziri Nnauye aliwasilisha hotuba iliyobainisha nafasi ya Tanzania katika kukuza TEHAMA. Picha na: TCRA.Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb.) akiwasilisha hotuba inayobainisha nafasi ya Tanzania katika kukuza TEHAMA hasa katika kusambaza huduma za mawasiliano kwa wote mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Maendeleo ya Mawasiliano Duniani (ITU-WTDC-2022) ulioandaliwa na Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU) na kufanyika mjini Kigali, Rwanda katika Kituo cha Mikutano cha Rwanda (KCC). Picha na: TCRAWashiriki wa Mkutano Mkuu wa Maendeleo ya Mawasiliano Duniani (ITU-WTDC-2022) wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari-Tanzania, Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb.) aliyoiwasilisha kuhusu nafasi ya Tanzania katika kukuza TEHAMA. Mkutano huo Mkuu uliandaliwa na Shirika la Mawasiliano Duniani-(ITU) na kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Rwanda (KCC), mjini Kigali, Rwanda. Picha na: TCRAWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb.) (kushoto) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Wizara Dkt. Jim Yonazi (kulia) katika kituo cha Mikutano-Rwanda Convention Centre jijini Kigali, Rwanda pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa Maendeleo ya Mawasiliano (ITU-WTDC-2022) ulioandaliwa na Shirika la Mawasiliano Duniani-ITU. Waziri Nape aliwasilisha hotuba ya nafasi ya Tanzania katika kukuza TEHAMA. Picha na: TCRA.Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari-Tanzania, Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb.) (wa tatu kulia kutoka ukutani) akishiriki pamoja na ujumbe wa Tanzania, mazungumzo na Mshauri Mwandamizi: Ubunifu na Ushirikiano wa Kidijitali-Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufini Bw. Aki Enkenberg, walipojadili ubadilishanaji wa mbinu bora katika utekelezaji wa miradi ya mabadiliko ya kidijitali, kuimarisha uwezo katika ujuzi wa kidijitali, kujenga mfumo-ikolojia bora wa uvumbuzi katika TEHAMA na kupata uungwaji mkono wa Ufini kwa Tanzania katika Baraza la ITU. Kikao hicho kilifanyika pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa Maendeleo ya Mawasiliano Duniani (ITU-WTDC-2022) ulioandaliwa na Shirika la Mawasiliano Duniani-ITU na kufanyika mjini Kigali, Rwanda. Picha na: TCRA.Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari-Tanzania, Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb.) akifuatilia mada, muda mfupi baada ya kuwasilisha hotuba ya nafasi ya Tanzania katika kukuza TEHAMA katika kusambaza huduma za mawasiliano kwa wote. Hotuba iliwasilishwa mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Maendeleo ya Mawasiliano Duniani (ITU-WTDC-2022) ulioandaliwa na Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU) na kufanyika mjini Kigali, Rwanda katika Kituo cha Mikutano cha Rwanda (KCC). Picha na: TCRAWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb.) akifuatana na Msaidizi wake akiwasili kwenye Kituo cha Mikutano cha Rwanda (KCC), kushiriki Mkutano Mkuu wa Maendeleo ya Mawasiliano Duniani (ITU-WTDC-2022); Waziri aliwasilisha mada kwenye mkutano huo juu ya maendeleo ya mawasiliano Tanzania na duniani. ITU-WTDC-2022 ni Mkutano unaowakutanisha nchi wanachama wa Shirika la Mawasiliano Duniani kujadili masuala mtambuka ya ukuzaji wa TEHAMA. Picha na: TCRAWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb.) akiwahutubia washiriki wa Mkutano Mkuu wa Maendeleo ya Mawasiliano Duniani (ITU-WTDC-2022) ulioandaliwa na Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU) na kufanyika mjini Kigali, Rwanda katika Kituo cha Mikutano cha Rwanda (KCC). Hotuba ilibainisha nafasi ya Tanzania katika kukuza TEHAMA hasa ufikishaji huduma za mawasiliano kwa jamii zisizofikiwa. Picha na: TCRAWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari-Tanzania, Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb.) (wa tatu kulia kutoka ukutani) akishiriki pamoja na ujumbe wa Tanzania, mazungumzo na Wawakilishi wa Kenya, kujadili masuala mtambuka ya ushirikiano katika sekta ya mawasiliano. Kikao hicho kilifanyika pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa Maendeleo ya Mawasiliano Duniani (ITU-WTDC-2022) ulioandaliwa na Shirika la Mawasiliano Duniani-ITU na kufanyika mjini Kigali, Rwanda. Picha na: TCRA.Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb.) (wa nne kutoka kulia), uliposhiriki mkutano wa mashauriano na wenzao wa Japan wakiongozwa na Naibu Waziri wa Uratibu wa Masuala ya Kigeni, Mhe. Yuji Sasaki na ujumbe wake, kujadili ushirikiano kwenye sekta ya mawasiliano baina ya nchi hizo mbili. Miongoni mwa maeneo yaliyopewa kipaumbele ni Mageuzi ya Kidijitali, kujenga uwezo katika TEHAMA na upokeaji wa teknolojia ya 5G. Katika mkutano huo, Waziri Nape aliambatana na ujumbe wa wataalam wa sekta ya mawasiliano walioongozwa na Katibu Mkuu-WHMTH Dkt. Jim Yonazi (wa tatu-kulia kutoka ukutani), Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Dkt. Jabiri Bakari (wa tatu kulia kutoka lensi), Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Bi. Justina Mashiba (wa kwanza kulia kutoka ukutani) na maafisa waandamizi wa Wizara na TCRA. Picha na: TCRAWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb.) (wa nne kutoka kulia), katika picha ya pamoja na ujumbe wa Japan ukiongozwa na Naibu Waziri wa Uratibu wa Masuala ya Kigeni Mhe. Yuji Sasaki (wa nne kutoka kushoto), baada ya kikao cha mashirikiano kwenye sekta ya mawasiliano baina ya Tanzania na Japan. Wengine ni Mkurugenzi wa TEHAMA WHMTH Bw. Mulembwa Munaku (wa kwanza kulia), Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Jabiri Bakari (wa pili kulia), Katibu Mkuu WHMTH Dkt. Jim Yonazi (wa tatu kulia), Mkurugenzi wa Masuala ya Sekta-TCRA Dkt. Emmanuel Manasseh (wa kwanza kushoto), Mtendaji Mkuu wa UCSAF Bi. Justina Mashiba (wa pili kushoto) na mgombea wa nafasi ya Mkurugenzi wa Viwango vya TEHAMA ITU-T Bw. Seizo Onoe (wa tatu kushoto). Picha na TCRA
Social Plugin