WATAFITI NELSON MANDELA WAJENGEWA UWEZO WA KUTUNZA BUNIFU ZAO

Ofisa Mwandamizi Utumishi na Utawala kutoka Brela Ndg.Raphael Mtalima wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) akielezea kuhusu Umiliki wa Uvumbuzi (Intellectual Property) katika warsha ya kuwajengea uwezo Watumishi na watafiti kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Juni 13 ,2022 Jijini Arusha.
Menaja Usimimazi wa Bunifu katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Ndg. Joseph Swai akielezea jambo katika warsha ya kuwajengea uwezo Watumishi na Watafiti wa Taasisi hiyo iliyoandaliwa kwa kushirikiana na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Juni 13 ,2022 Jijini Arusha.

Ofisa Mwandamizi Utumishi na Utawala wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Ndg.Raphael Mtalima (kushoto) akimsikiliza Menaja Usimimazi wa Bunifu katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Ndg. Joseph Swai (kulia) wakati wa warsha ya kuwajengea uwezo Watumishi na Watafiti kutoka Taasisi hiyo Juni 13 ,2022 Jijini Arusha.

..................................................................

Watumishi na watafiti kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela wajengewa uwezo wa namna ya kutunza tafiti na bunifu zao kupitia warsha ya siku moja iliyoandaliwa kwa ushirikiano na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Juni 13 ,2022 Jijini Arusha.

Akizungumza katika warsha hiyo Ofisa Mwandamizi Utumishi na Utawala kutoka Brela Ndg. Raphael Mtalima alisema kuwa wabunifu na wavumbuzi wanavumbua bunifu zao lakini hawajui wazilinde vipi na hivyo kutokufaidika na matunda ya vumbuzi hizo.

Anazidi kueleza kuwa, katika kuhakikisha wabunifu na watafiti wanapata uelewa kuhusu Umiliki wa Uvumbuzi (Intellectual Property ) Brela imeamua kutoa elimu katika vyuo vitano vilivyopo jijini Arusha ikiwemo Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela iliyojikita katika masuala ya kisayansi.

"Tunawajengea uwezo wabunifu wajue umuhimu wa kuendelea na tafiti zao na kuzisajili BRELA kwa ajili ya kunufaika nazo hapo baadaye"amesema Ndg. Raphael.

Naye Mkuu wa Idara ya Utafiti na Ubunifu katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela , Dr. Edna Makule alisema warsha hiyo ina manufaa makubwa kwa watafiti na wabunifu kutoka katika taasisi hiyo kwa kuwa tayari imefanya tafiti na bunifu mbalimbali zilizofikia hatua ya kulindwa, kupitia elimu waliyoipata itasaidia kupiga hatua zaidi katika kulinda bunifu hizo.

Kwa upande wake Mwanafunzi anayechukua masomo ya Shahada ya Uzamivu (PhD), Isack Kandola alisema amejifunza mambo mengi kupitia warsha hiyo na kuahidi kufanyia kazi na kutoa elimu kwa wengine waliokosa fursa ya kuhudhuria ili kulinda bunifu zao zisiibiwe.

Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela ni Taasisi inayotoa elimu kwa ngazi ya Shahada ya Uzamili( Masters) na Uzamivu (PhD) katika masuala ya sayansi na teknlojia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post