Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe.Faidha Salim akifungua mafunzo kuhusu Udhibiti wa Sumukuvu kwa Mazao ya Mahindi, Karanga pamoja na bidhaa zake kwa wafanyabiashara, Wasafirishaji na Wasindikaji leo Juni 1,2022 wilayani humo.
Baadhi ya wafanyabiashara, Wasafirishaji na Wasindikaji kutoka katika Wilaya ya Itilima wakifuatilia mafunzo kuhusu Udhibiti wa Sumukuvu kwa Mazao ya Mahindi, Karanga pamoja na bidhaa zake yaliyotolewa na TBS katika wilaya hiyo leo Juni 1,2022.
********************
NA MWANDISHI WETU
Usalama wa chakula unakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na uchafuzi wa sumukuvu ambayo husababisha madhara ya kiafya na hata kiuchumi.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe.Faidha Salim wakati akifungua mafunzo kuhusu Udhibiti wa Sumukuvu kwa Mazao ya Mahindi, Karanga pamoja na bidhaa zake kwa wafanyabiashara, Wasafirishaji na Wasindikaji kutoka katika Wilaya ya Itilima.
Amesema Serikali imekuwa ikifanya jitihada za kukabiliana na uchafuzi wa sumukuvu katika mazao wakati yanapokuwa shambani, wakati wa uvunaji, usafirishaji, uhifadhi na usindikaji hivyo kupitia mafunzo haya yanayotolewa na TBS yatawajenga wengi.
Aidha amesema TBS imekuwa ikifanya jitihada za kulinda afya ya jamii kwa kudhibiti usalama na ubora wa bidhaa za chakula nchini ikiwa ni pamoja na mahindi, karanga na bidhaa zake.
"Naishukuru TBS kupitia Mradi wa Kudhibiti Sumukuvu Tanzania- TANIPAC kwa kutoa kipaumbele katika suala la kuelimisha jamii ya Wilaya ya Itilima juu ya usalama wa chakula hususan katika udhibiti wa sumukuvu ili kuweza kukabiliana na tatizo hilo". Amesema
Social Plugin