Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAZIRI NDAKI AWATAKA WATANZANIA KUTEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII VILIVYOPO NCHINI


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki akiwa katika maonyesho ya Kill Fear yaliyofunguliwa leo jijini Arusha.

Na Rose Jackson,Arusha


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki ametoa wito kwa watanzania kutembelea vifutio vya utalii vilivyopo hapa nchni kwani masharti yaliyokuwepo awali yamepungua.


Mhe Ndaki ameyasema hayo leo jijini Arusha kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii Pindi Chana wakati akizindua maonyesho ya Karibu Kili fear 2022 yalioanza leo katika viwanja vya Kisongo Magereza jijini Arusha.


Amesema watanzania na watalii wanapaswa kutembelea vivutio vya kiutalii kwa kiwa maeneo hayo yanafikika ikiwa ni pamoja na masharti kupungua.


"Nitoe wito kwa watanzania na watalii kutembelea vivutio vyetu vilivyopo hapa nchi kwani maeneo yanafikika lakini pia masharti yamepungua kwani Covid 19 imeshaisha na ndiyo ilikuwa inafanya kuwepo masharti",aliongeza.

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Mohamed Mansour amesema kwa upande wa Zanzibar wanamuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan na wameweza kujumuika na Tanzania bara kutangaza utalii.


"Sisi Zanzibar tumeamua kuungana na Tanzania Bara katika maonyesho haya ili kuunga mkono jitiada za kutangaza Royal Tour,"aliongeza Mansour.


Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela amesema kuwa Arusha ni salama na itaendelea kuwa salama na kama mkoa agenda yao ni kkuifanya iwe kitovu cha matukio makubwa.


Mongela amesema kuwa maonyesho hayo yanatangaza nchi na jumuiya ya Afrika mashariki Arusha inafikiri jinsi ya kutengeneza mshikamano ambao utauza vivutio kitaifa ili nchi iweze kunufaika zaidi.


Mkurugenzi wa Kili fear Company Ltd Dominic Shoo ambao ndio waandaaji wa maonyesho hayo amesema kuwa wmaefanya uzinduzi rasmi kuonyesha dunia kuwa Kuna utalii na kwamba kuna mengi ya kujifunza.


Maonyesho hayo yanashirikisha wadau mbalimbali wa utalii kutoka nchi mbali mbali duniani ambayo yanalenga kutanga vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com