Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akizungumza na waandaaji wa tamasha la Nandete Majimaji Festival la kutangaza utalii wa utamaduni na malikale, katika kikao kilichofanyika ofisini kwake jijini Dodoma leo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akizungumza na waandaaji wa tamasha la Nandete Majimaji Festival la kutangaza utalii wa utamaduni na malikale, katika kikao kilichofanyika ofisini kwake jijini Dodoma leo. Kulia ni Mbunge wa Kilwa Kaskazini Mkoani Lindi, Mhe. Francis Ndulane.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na waandaaji wa tamasha la Nandete Majimaji Festival la kutangaza utalii wa utamaduni na malikale, katika kikao kilichofanyika ofisini kwake jijini Dodoma leo. Wa tatu kutoka kulia ni Mbunge wa Kilwa Kaskazini Mkoani Lindi, Mhe. Francis Ndulane.
**********************
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amesema Wizara ya Maliasili na Utalii iko tayari kutoa ushirikiano kwa wadau wanaofanya jitihada za kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kuandaa matamasha ya kutangaza utalii wa utamaduni na malikale.
Ameyasema hayo leo ofisini kwake jijini Dodoma alipokutana na waandaaji wa tamasha la Nandete Majimaji Festival litakalofanyika kuanzia tarehe 13 mwezi Agosti 2022 na kumalizika 15 mwezi Agosti 2022 katika Kata ya Kipatimo Kijiji cha Nandete Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi.
Tamasha hilo lenye kauli mbiu ya “Majimaji Tujiandae Kuhesabiwa”litahusisha mashindano ya mbio, mashindano ya mpira wa miguu na mashindano ya ngoma za asili ambapo washindi watapewa zawadi mbalimbali.
Social Plugin