*************
NA EMMANUEL MBATILO
KLABU ya Yanga leo imekabidhiwa kombe lao la Ligi Kuu Tanzania Bara NBC mara baada ya kutangazwa mabingwa wa ligi hiyo hivi karibuni.
Yanga Sc imekabidhiwa kombe hilo leo Sokoine mkoani Mbeya ambapo walikuwa wanacheza mchezo wao wa 29 bila kufungwa hivyo na kubakia na mechi moja wamalize ligi bila kufungwa.
Yanga Sc wamecheza na Mbeya City na kulazimishwa sare ya 1-1, mchezo ambao ulijawa na hisia za mashabiki ambao waliujaza uwanja huo kushuhudia Yanga ikikabidhiwa kombe hilo.
Social Plugin